Nashauri Ndoa ifundishwe kama somo shuleni au vyuoni

Nashauri Ndoa ifundishwe kama somo shuleni au vyuoni

General Nguli

JF-Expert Member
Joined
Apr 22, 2022
Posts
1,190
Reaction score
2,508
Nashauri serikali iweze kuanzisha somo la Ndoa kwa kila mmoja anaekaribia kuingia humo. Hakika wengi wetu tunaingia katika ndoa bila kujua bila kuelewa ndoa nakujikuta tunazama kupitia Mihemko.

Ndoa ni familia. Familia ndo jamii na jamii ni Nchi. Hakika kuna haja ya Serikali kuwekeza kwenye Somo la ndoa. Kwa Nchi yetu ukitoa vifo vya ajali mbali mbali basi zinafuatia vifo vya Mahusiano. Hakika kwenye hili kunahitajika Syllabus mtu afaulu ndipo aingie kwenye Ndoa.

Nisiseme sana ila Wadau watakuwa wameelewa.
 
Nashauri serikali iweze kuanzisha somo la Ndoa kwa kila mmoja anae karibia kuingia humo.
Hakika Wengi wetu tunaingia katika ndoa bila kujua bila kuelewa ndoa nakujikuta tunazama kupitia Mihemko.
Ndoa ni familia...Familia ndo Jamii na Jamii ni Nchi.
Hakika kuna haja ya Serikali kuwekeza
kwenye Somo la ndoa.
Kwa Nchi yetu ukitoa vifo vya ajali mbali mbali basi zinafuatia vifo vya Mahusiano.Hakika kwenye hili kuna hitajika Syllabus mtu afaulu ndipo aingie kwenye Ndoa.
Nisiseme sana ila Wadau watakuwa wameelewa.
Sisi tunafundisha na hamji kusoma
 
Hata ikifundishwa bado ndoa ni fumbo (..1] wapo walosoma (wasio soma)sana na ndoa zimewapendezea/vuruga ..b)wapo walosoma kiasi na ndoa zimewapendezea/vuruga.......c) wapo wasiosoma na ndoa zimewapendezea/vuruga])

Changamoto
1. Kwenye ndoa usitegeme 100% kumbadilisha mwenzio tabia zake (Ni ngumu sanaa)
2. Was kumpenda mwenzio 60% na inayobaki ni kwa watoto 30% na ndugu 10%
3. Simu zimekuwa nongwa .................(mada ingine kabsaa)
4. Usiwaze mwenzio ataridhika 100% na (kujamiiana) men are men and women are women .... mwanaume hajawahi kuridhika na lile tendo kutoka kwa mtu mmoja tu
5. Zipo tabia za kuvumilia na zipo zisizo vumilika (jitathimini mwenyewe)
6. Umbali wa wanandoa waishipo (mada mtambuka)
7. Ubinafsi ndo tatizo kubwa sana
8. tafta furaha yako ya maisha, usiwaze ndoa kwa kulazimishwa .... hadi mnakutana kila mmoja ashapitia maisha fulaniii ayajuayo...anaweza kukusimulia ama ikawa siri kwake
 
Haitakuwa na maana, labda kwa mfumo mwingine maana watu wanasoma kuhusu rushwa tangu primary lakini hali ni ileile.
 
Ushauri wa kijinga
20230726_165738.jpg
 
Back
Top Bottom