Nashauri serikali itilie maanani mchezo wa Long Jump naamini tutaweza na ijenge viwanja vya mazoezi

Nashauri serikali itilie maanani mchezo wa Long Jump naamini tutaweza na ijenge viwanja vya mazoezi

N'yadikwa

JF-Expert Member
Joined
Aug 10, 2014
Posts
7,427
Reaction score
10,905
Wakati nikikua mchezo wa kuruka kwa upondo na ule wa kuruka kawaida sambamba na mchezo wa kurusha mkuki na vitu vizito ilikuwa inafanyika na watu walikuwa wanafanya vizuri.

Ukizingatia kwamba Wakenya tayari wamejitambulisha kwa mchezo wa riadha; sisi hapa kwetu Tanzania bado hatujakuwa na mchezo unaotutambulisha vema; nashauri sasa tujaribu michezo hii kwa serikali kuitilia mkazo ikiwa ni pamoja na kujenga viwanja vyake vikubwa hasa kwenye miji mikubwa kama Mwanza Dar Dodoma Arusha na Mbeya japo kwa kuanzia.

Tuseme ukweli Tanzania kwenye diplomasia ya michezo bado hatufanyi vizuri kwa kuwa hatuna timu za mchezo wowote zinazoenda wala kushinda medali kwa kiwango chochote cha kuridhisha tangu enzi zile za riadha ya kina Nyambui na Filbert. Serikali uchaguzi ukiisha tafadhali mliweke hili kwenye ajenda, tunapenda kuwa na vizazi vyenye furaha na umoja kwani michezo hutuleta pamoja. Na michezo sio soka pekee. Kuna watu wanapenda aina hiyo na michezo; ipatiwe kipaumbele bila kusahau mieleka.

Nawasilisha.
83eecbc7-60e5-4a10-8de7-32ae5decbb35.png
2007_Military_World_Games_long_jump.jpg
285px-Pole_Vault_Sequence_4.jpg
Hammerthrow_wire.jpg
 
Nyumbani niliwai kuona picha ya mchezo wa high jump ukifanyika nchini, tena ilikuwa songea hiyo picha ndio ilipigwa
 
Back
Top Bottom