Nashauri shule zote zifutwe ili kukuza ajira

BICHWA KOMWE -

JF-Expert Member
Joined
Jul 21, 2022
Posts
6,373
Reaction score
16,073
Huko Tanganyika unaweza ukasoma miaka na miaka mpaka mgongo ukapinda, halafu ukimaliza kusoma unaambiwa kawe KONDAKTA.

Na usiombe uwe kondakta mwenye digriii, utasimangwa mpaka na sisimizi. Ukikodoa jicho unaona kila mtu anakuzomea. Unaamua kuvaa miwani myeusi.

Utafiti wa kitaalamu unaonesha kuwa, hakuna haja ya kusoma hadi chuo kikuu ili uwe KONDAKTA. Unaweza ukawa KONDAKTA bila kufika hata FOM FOO. Unaingia mzigoni unakusanya maokoto kiulani.

Nashauri shule zote nchini zifungwe, hatuwezi kuwa tunalipa makodi mengi, tunalipa walimu, tunalipa mabilioni ya kusomesha wanavyuo, tunajenga majengo ya mapesa mengi, KWA AJILI YA kuzalizisha MAKONDAKTA.

Kama ni UKONDATA tutajifunza hata kwenye google. Uki-google magari ya kwenda gomzi unapata material yote unajisomea unapata ujuzi wa kuwa KONDAKTA.

Hili nalo MKALITIZAME, tuna mambo mengi ya kufanya, hatuwezi kuwa na nchi inayotumia matrilioni kusomesha MAKONDAKTA.

Ni bora hizo hela tujenge barabara za lami ili MAKONDAKTA wapite na magari yao bila bughudha. Hii itakuza ajira.
 
Nani alikwambia unasoma ili uajiriwe, unasoma ili uweze kupambana na mazingira !! Shule ndo zinazozalisha kila kitu unasema ukondakta utajifunza kwenye google 😂😂 halafu unasema shule zifutwe huko google utaenda kusomaje hata kama kuna akili bandia inaweza kukusomea bado unahitaji kusoma shule ili utatue changamoto zako za kila siku.

Huyo unayemuita dereva lazima akasome ili aendeshe gari atajuaje alama za barabarani kama hajasoma!! Kondakta chenji atarudishaje ?

Shule ni sehemu ya maisha yetu
 
Nani alikwambia unasoma ili uajiriwe, unasoma ili uweze kupambana na mazingira !! Shule ndo zinazozalisha kila kitu unasema ukondakta utajifunza kwenye google [emoji23][emoji23] halafu unasema shule zifutwe huko google utaenda kusomaje hata kama kuna akili bandia inaweza kukusomea bado unahitaji kusoma shule ili utatue changamoto zako za kila siku.

Huyo unayemuita dereva lazima akasome ili aendeshe gari atajuaje alama za barabarani kama hajasoma!! Kondakta chenji atarudishaje ?

Shule ni sehemu ya maisha yetu
Sio lazima tusomee shuleni, hata vituo vya polisi vinaweza kufanywa kuwa maeneo ya mafunzo na polisi wakawa walimu.

Waalifu wote wakafundishwa kwa lazima na kupewa ajira kama kifungo kulingana na kosa.

Shule zikifungwa madarasa yana matumizi mengi mengine, kama kuwapangisha wazawa wasio na makazi maalum nk.
 
A
Eti
Primary 7 yrs
Secondary 4 yrs
Advanced secondary 2 yrs
University 3 yrs minimum.
Total 16 yrs hapo umekwenda full.
Miaka 16 unasomea ubodaboda ambao unaweza kufundishwa kwa dk 30 tu.
Akili ndogo kama hizi ni mzigo mkubwa sana kwa Taifa.
 
L
Mwenye akili ndogo ni yule anaspend miaka zaidi ya 16 kusoma then anakuwa bodaboda.
Kama angetaka kuwa boda si angeanza alipomaliza primary
Unasomea kitu ambacho hutakitumia kwa maslahi yako na Taifa huoni kuwa ni uwehu?
Upeo wako ni mdogo sana! Wewe unadhani kusoma ni Kwa ajili ya kuajiriwa tu!
Fanya uchunguzi utagundua kuwa Badaboda mwenye degree na Bodaboda wa Darasa la Saba wanatofauti kubwa sana!
 
Sio lazima tusomee shuleni, hata vituo vya polisi vinaweza kufanywa kuwa maeneo ya mafunzo na polisi wakawa walimu.

Waalifu wote wakafundishwa kwa lazima na kupewa ajira kama kifungo kulingana na kosa.

Shule zikifungwa madarasa yana matumizi mengi mengine, kama kuwapangisha wazawa wasio na makazi maalum nk.
Hicho unachokisemea tayari inakua imekua shule umebadilisha tu mukhtadha , umezungumzia kujifunza humo !!

Shule ni mahali ambapo watu hujifunza mambo mengi ambayo huwasaidia katika kuyakabili maisha hata kupata elimu juu ya jambo fulani pia ni majengo.
Maeneo ya mafunzo ndo itakua shule sasa. 😂
 
Huko Tanganyika unaweza ukasoma miaka na miaka mpaka mgongo ukapinda, halafu ukimaliza kusoma unaambiwa kawe KONDAKTA.

Na usiombe uwe kondakta mwenye digriii, utasimangwa mpaka na sisimizi. Ukikodoa jicho unaona kila mtu anakuzomea. Unaamua kuvaa miwani myeusi.

Utafiti wa kitaalamu unaonesha kuwa, hakuna haja ya kusoma hadi chuo kikuu ili uwe KONDAKTA. Unaweza ukawa KONDAKTA bila kufika hata FOM FOO. Unaingia mzigoni unakusanya maokoto kiulani.

Nashauri shule zote nchini zifungwe, hatuwezi kuwa tunalipa makodi mengi, tunalipa walimu, tunalipa mabilioni ya kusomesha wanavyuo, tunajenga majengo ya mapesa mengi, KWA AJILI YA kuzalizisha MAKONDAKTA.

Kama ni UKONDATA tutajifunza hata kwenye google. Uki-google magari ya kwenda gomzi unapata material yote unajisomea unapata ujuzi wa kuwa KONDAKTA.

Hili nalo MKALITIZAME, tuna mambo mengi ya kufanya, hatuwezi kuwa na nchi inayotumia matrilioni kusomesha MAKONDAKTA.

Ni bora hizo hela tujenge barabara za lami ili MAKONDAKTA wapite na magari yao bila bughudha. Hii itakuza ajira.
Serikali iwekeze sana kwenye elimu ya ufundi
 
Hicho unachokisemea tayari inakua imekua shule umebadilisha tu mukhtadha , umezungumzia kujifunza humo !!

Shule ni mahali ambapo watu hujifunza mambo mengi ambayo huwasaidia katika kuyakabili maisha hata kupata elimu juu ya jambo fulani pia ni majengo.
Maeneo ya mafunzo ndo itakua shule sasa. [emoji23]
Na iwe ivyo, tunatumia ghalama kubwa kujenga majengo mengi wakat vituo vya polisi vipo.

Badala ya kukimbizana mtaani na kuhifadhi vibaka na wavuta bangi kwny selo zao, sasa ni muda polis nao wabadilishiwe majukum.

Sioni kama jukumu walilonalo kwa sasa linawafaa.
 
Eti
Primary 7 yrs
Secondary 4 yrs
Advanced secondary 2 yrs
University 3 yrs minimum.
Total 16 yrs hapo umekwenda full.
Miaka 16 unasomea ubodaboda ambao unaweza kufundishwa kwa dk 30 tu.
Tunapoteza sana muda kwenye HAMNA.
 
Back
Top Bottom