Nashauri tanzania iingie mkataba wa haraka na congo vijana wa Kitanzania wapate ajira ya haraka

Cobra70

Senior Member
Joined
Jan 2, 2020
Posts
178
Reaction score
376
Ninawaza kwa Sauti ya chini sana nikiwa nakunywa taratibu kiburudisho kisicholewesha.

Ni hivi vijana wengi wa Kitanzania wamekuwa na ndoto au matamanio ya kujiunga na jeshi la JW na hivyo kupelekea wengine kushindwa vigezo vya kujiunga na jeshi hilo na wengine kudondokea kwenye mikono ya matapeli kwa ahadi ya kutafutiwa nafasi ya kozi katika jeshi hilo.

Point yangu ni hivi wanaume wa Congo wameonekana ni dhaifu na waoga kuilinda nchi yao, Je mnaonaje mkiwapa mafunzo ya JW vijana wetu wote ambao hawana kazi na waliomaliza vyuo ambao ni wavivu kazi yao ni kusubiria ajira za serikali ili kwenda kule kuwasaidia waCongo kulinda mali zao kwa mkataba mnono wa kuinua uchumi wetu?

Kwa point za hapo juu suala la ajira tutakuwa tumelitibu kwa kiasi chake na pia uchumi wetu utakuwa kwa kasi sana. Akili za warwanda na waganda nahisi waliwaza kama mimi ahsante na hapo tutakuwa tumewapiga spana.
 
Umewaza pia siku kazi yao ikikamilika na kurudi nyumbani itakuaje?
Hapa naongelea kuwahudumia na nchi yetu itaweza kuepuka waasi ndani ya jeshi na nchi??
Kwa maana hapa wapo pia watakaorudi na mitazamo tofauti na viapo vyao.
Kwa ishu ya Congo kwa upande wangu, kwa sababu m23 wameamua kutumia Vita kua njia ya kazi zake Basi na Jeshi la Congo na majeshi ya amani yatumie nao silaha kuwapiga in full Force. Majibu yatapatikana kwa haraka zaidi tofauti na zile jitihada za mazungumzo.
 
Hao vijana wa kitanzania wataobahatika kushiriki katika zoezi tajwa hapo juu, pindi jukumu litakapo kamilika/mkataba wa ulinzi EDRC kumalizika, watarudi nchini kama raiya au askari? JW watakua na mkakati gan juu yao? Maana watakuwa si raiya tena bali ni askar wa vita(kanuni kuu kwao ni mapigo na mwendo). Hivyo, naweza sema wazo husika ni zuri katika muktadha wa ajira kwa vijana ila hasara yake ni kubwa mno, linaweza litumbukiza Taifa kwenye machafuko yasiyokuwa na ukomo kama vijana husika watakaporudi nchini na kupuuzwa(kuachwa bila ajira).

Japo JW kupitia kamandi ya JKT katika wing yake ya SUMA-JKT wanakampuni ya Ulinzi. Wanaweza kujitanua kimajukumu ya Ulinzi na Usalama kwa kuajiri vijana na kuwapatia mafunzo ya kijeshi yatakayowawezesha kufanikisha zoez la ulinzi kwa wepesi nchini DRC, na watakaporud nchi wataendelea kuwa waajiriwa wa SUMA-JKT.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…