Nashauri tuungane kukataa kusapoti kazi, biashara za Wasanii Machawa wa Kisiasa

Katika hili huwa namushemimu sana Kiba, hata akipanda jukwaa la CCM anafanya yake bila shombo kwa wapinzani...unaona kabisa kapanda kufanya kazi iliyompeleka na hana tabia ya uchawa maana anazijua athari zake. Mondi hapa ndo pamefanya nipishane naye na asiposhtuka itamuharibia mno huko tuendako, asome alama za nyakati kupitia msanii wake Zuchu.
 
Watu 300 wanaopiga mavuvuzela humu ndio wasusie kazi za wasanii? Then?
 
Wazo zuri
 
Peleka kule X (Twitter) kina Maria watatoa sapoti ya kutosha.
 
Watanzania hawawezi kuungana kwa chochote kwa sasa. Ndio kwanza wanazidi kugawanywa, kujigawa kugawanyika kupitia vyama, dini, kabila, itikadi, pesa, propaganda, uchawa, kupandikizwa chuki na wengi hawajitambui hata akitokea kiongozi mzuri ni mtu wa aina gani hawatamtambua.
 
Ni kweli kuna mgawanyiko, lakini historia inaonesha Watanzania waliweza kuungana wakati wa harakati za uhuru, kupinga udikteta na hata majanga ya kitaifa.

Kumbuka Mgawanyiko si wa milele, uelewa pia unakua, na kizazi kipya kinaanza kuhoji na ndio maana kuna baadhi wameitwa Wasaliti na kupotezwa.

Umoja unaanza na wachache wanaojitambua.
 
Hela ya kulq utawapa ww hivi bichwa lako lina akili kweli
 
Naam, nadhani hajali fikiria hili, so that campaign can never succeed at all. 😎
Siyo lazima kila mtu aanze kwa kuelewa au kujali, lakini harakati nyingi zimefanikiwa kwa sababu ya uvumilivu na msimamo wa waliotangulia
 
Watu wanatekwa msanii hajihusishi ila akisikia ccmu inakosolewa anajitokeza na kutoa propaganda eti wapinzan wataleta vita
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…