Nashauri Vyeti vya elimu ya juu vitumike kama dhamana ya wasomi kupewa mikopo

zubedayo_mchuzi

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2011
Posts
4,873
Reaction score
1,217
VYETI VYA ELIMU YA JUU VITUMIKE KAMA DHAMANA YA WASOMI KUPEWA MIKOPO YA KUJIKWAMUA.

Habari jumapili Wana JF wote kwa ujumla.Jamani nimekuwa nikifikiria muda mrefu sana ni kwanini vyeti vya elimu ya juu visitumike kama dhamana ya kuwapa mikopo wasomi wetu wanao maliza na kukutana ukata wa ajira mtaani.Serikali imekuwa ikihimiza tu wasomi wanaomaliza watumie ujuzi wao kujipatia kipato bila kuwa wezesha.

Kuna haja tena kubwa sana kwa serikali kuliangalia hili kwa mapana zaidi kwa sababu huwezi ukamaliza chuo na ukajiajiri hivi hivi, bila kupewa mtaji,ili japo upate pa kuanzia.Kwa wale wanaotoka kwenye familia zenye uwezo wao wana hatua moja mbele zaidi tofauti na sisi wa familia duni.

Tanzania inazalisha wasomi wengi ambao hawana ajira na Serikali haitaki kutafuta njia mbadala ya kulikwamua kundi hili.Zaidi ya kuimba wasomi mjiajiri mjiajiri.

Ili kundi hili wasomi lipate pa kuanzia serikali,Taasisi binafsi za mikopo kuweka utaratibu wa kuwapa mikopo kwa DHAMANA YA VYETI VYAO.

Na hapa itawahusu wale wasomi wasio na ajira tu ndo wawezeshwe kama wewe umewezeshwa mpe nafasi na mwenzio ajikwamue

Naomba tujadiri hili kwa mapana zaidi..vijana wengi wanaumia mtaani bure kwa kukosa fursa tu za mitaji.

================
UPDATE - May 2014:

Waziri Kabaka kalifanyia kazi hili - https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...wasomi-vyeti-kuwa-dhamana-ya-mikopo-crdb.html
 
Mtu akikuachia cheti chake na kutolipa mkopo then what? Utauza cheti?

mkuu ungefunguka ili nikuelewe.siyo kuniuliza swali moja kwa moja.

sidhani kama atakimbia na mkopo akaacha cheti
 
Hahahahahahha hahahhahahahaha hhahhhahahaha hahahahahahasha,,,kama ingekuwa hivyo tungeona maduka mengi ya jumla na rejareja yakiuza vyeti.



mkuu ungefunguka ili nikuelewe.siyo kuniuliza swali moja kwa moja.

sidhani kama atakimbia na mkopo akaacha cheti
 
ili kupata mkopo,lazima uwe na collateral yenye thamani na mkopo unaotaka,incase ukishindwa kulipa,collateral uloweka inauzwa.sasa,cheti utathaminishaje? Now,kuna mikopo ya biashara ndogondogo,hata kama huna collateral unapewa but uwe na biashara ambayo ni permanent.equity bank wanatoa hiyo.nenda jukwaa la biashara,utapata maelezo mazuri ya mikopo.
 
ni wazo zuri lakini cheti ni kama kitambulisho chako,kuweka bondi haina maana kwani ukishindwa kulipa deni then hawana namna ya kufanya kuhusu cheti chako....na wewe kutokuwa na cheti sio kwamba utalala njaa...wengi vyeti vimepotea lakini wanafanya kazi tena za kuajiriwa....thamani ya elimu yako ipo kichwani mwako sio kwenye cheti,cheti ni utambulisho tu tena wa kitu kisichoonekana.
 
mkuu ungefunguka ili nikuelewe.siyo kuniuliza swali moja kwa moja.

sidhani kama atakimbia na mkopo akaacha cheti

Usiniambie unachodhani. Una ruhusiwa kudhani mauzauza yoyote.Niambie unachojua.

Nifunguke vipi wakati swali linajieleza?

Wewe mtoa mkopo. Umenikopesha mshiko. Collateral cheti. Nimekuachia jumla, sijalipa deni hata senti tano ila nimefanya mpango nimepata cheti kingine. Nilichokupa sikihitaji. Nimeripoti kimepotea.

Wewe na collateral yako ya cheti changu cha karatasi mkononi mwako utafanya nini?

Utakiuza ili kufidia hasara?

Goes back to show you wabongo wanavyothamini makaratasi ya hati za shule.

Where Nyani Ngabu at?
 
Last edited by a moderator:

Hao waliotoa hilo wazo ni kati ya hao graduates?

Halafu tunaambiwa wabunge lazima wawe graduates.

With graduates like these, who needs illiterates?
 
Mara nyingi sana huwa nafikiri hili wazo kuwa vyeti hivyo kwa vile vyenye sifa nzuri kuanzia vya SECONDARY haviwezi kutumika kuomba mkopo na kuliko kutaka hati za nyumba wakat wengi hawana na wakati hivyo vyeti vina thaman zaidi ya nyumba.
 
Ukipata benki wanayokubali vyeti vya sekondari tustuane mi changu hata kwenda ualimu hakikubalansi, sasa naona mkopo utakuwa matumizi mbadala wenye manufaa.
 
Unahitaji elimu ya masuala ya fedha na mikopo mkuu.....kumbuka sehemu ya Pesa wanazokopesha watu c za kwao ni za wateja wa hiyo bank sasa ukikopa halafu ukishindwa kulipa hiyo pesa unataka benki wauze cheti chako ili Pesa yao irudi...pia kumbuka huwezi kuifahamu au kuwa mfanyabiashara mzuri kwa kuisomea darasani au ukifaulu vizuri masomo ya biashara basi wewe ni mfanyabiashara mzuri ha ha ha....biashara ni elimu ya vitendo na sio nadharia ndo maana wasomi wengi sio wafanyabiashara hapa ulimwenguni ingawa wengine wana PhD za masomo ya biashara...njia nzuri ya kuifahamu biashara ni kuifanya na sio kuisomea peke yake
 
kuna benk kama CRDB wanakubali kuweka dhamana ya vyet lakin kuanzia ngazi ya degree na si vingnevyo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…