zubedayo_mchuzi
JF-Expert Member
- Sep 2, 2011
- 4,873
- 1,217
VYETI VYA ELIMU YA JUU VITUMIKE KAMA DHAMANA YA WASOMI KUPEWA MIKOPO YA KUJIKWAMUA.
Habari jumapili Wana JF wote kwa ujumla.Jamani nimekuwa nikifikiria muda mrefu sana ni kwanini vyeti vya elimu ya juu visitumike kama dhamana ya kuwapa mikopo wasomi wetu wanao maliza na kukutana ukata wa ajira mtaani.Serikali imekuwa ikihimiza tu wasomi wanaomaliza watumie ujuzi wao kujipatia kipato bila kuwa wezesha.
Kuna haja tena kubwa sana kwa serikali kuliangalia hili kwa mapana zaidi kwa sababu huwezi ukamaliza chuo na ukajiajiri hivi hivi, bila kupewa mtaji,ili japo upate pa kuanzia.Kwa wale wanaotoka kwenye familia zenye uwezo wao wana hatua moja mbele zaidi tofauti na sisi wa familia duni.
Tanzania inazalisha wasomi wengi ambao hawana ajira na Serikali haitaki kutafuta njia mbadala ya kulikwamua kundi hili.Zaidi ya kuimba wasomi mjiajiri mjiajiri.
Ili kundi hili wasomi lipate pa kuanzia serikali,Taasisi binafsi za mikopo kuweka utaratibu wa kuwapa mikopo kwa DHAMANA YA VYETI VYAO.
Na hapa itawahusu wale wasomi wasio na ajira tu ndo wawezeshwe kama wewe umewezeshwa mpe nafasi na mwenzio ajikwamue
Naomba tujadiri hili kwa mapana zaidi..vijana wengi wanaumia mtaani bure kwa kukosa fursa tu za mitaji.
================
UPDATE - May 2014:
Waziri Kabaka kalifanyia kazi hili - https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...wasomi-vyeti-kuwa-dhamana-ya-mikopo-crdb.html