Nashauri Wagombea Urais wawe wamepitia Chuo cha Taifa cha Ulinzi (NDC)

Nashauri Wagombea Urais wawe wamepitia Chuo cha Taifa cha Ulinzi (NDC)

Kama wanavyopelekwa Wakuu wa Mikoa, Wilaya na Watendaji wengine nashauri pia watu watakaotaka kugombea Urais baada ya majina yao kupitishwa na tume waende kozi ya NDC hata kwa wiki tatu.

Hii inaweza kufanywa na hata kwa Baraza la Mawaziri.
Tabia ya mlafi/ufisadi haibadiliki hata akipitia chuo chochote cha mafunzo. Sisi wananchi tusikubali visingizio vya viongozi wetu. Kiongozi ameharibu kazi tunasema hajapitia mafunzo fulani. Kiongozi anayeharibu kazi anatakiwa awajibishwe ipasavyo. Kiongozi wa kisiasa anaomba kazi yenye mwenyewe. Kiongozi wa serikalini ndio wanapitia kwenye vyuo mbalimbali ili kuongeza ujuzi na kupandishwa vyeo. Mtu anayeomba nafasi ya uongozi lazima awe anauelewa wa kazi anayoomba, na akiharibu kazi awe tayari kukubali matokeo yake.
 
"mwafrika hawezi kujitawala"Botha

"Mwafrika hawezi kuweka mipango ya miaka miwili mbele "Botha

"Nani asiyejua kuwa uafrika ni ufinyu na uduni wa fikra"Botha

Tanzania ndio taifa pekee ambalo wajinga ndo viongozi na waerevu ndo wafuasi uliwahi ona wapi au kusoma wapi mageuzi ya taifa katika nyanja zote yaliletwa na vilaza yaani Karne hii ya sayansi na teknolojia sifa ya kuwa kiongozi ni kujua kusoma na kuandika alafu mtegemee kupata maendeleo.

Siku mwafrika akishinda vita dhidi ya ubinafsi wake ndio siku ya mageuzi ya kweli ya kifrika yatakuja katika bara la Afrika
 
Usiwaamini hao "wadudu". Usidanganyike!

Tambua tu kwamba hizo kozi na vyeti havina uhusiano na weledi, uaminifu wala uzalendo - hakuna tija kwa kazi wala faida kwa taifa. Ni mambo ya "gizani"
 
Back
Top Bottom