Nashauri Wanajeshi mnapokuja kwenye biashara za kiraia msije kikundi na kuvaa magwanda

sanalii

JF-Expert Member
Joined
Oct 1, 2018
Posts
1,639
Reaction score
5,767
Mimi binafsi naona ni ubabe wa usiofaa wa baadhi ya wanajeshi, mtu anakuja ofisini kwako kavaa kiraia.

Mnafanya biashara vizuri, Ikitokea biashara imeenda kinyume siku akija kueleza matatizo anakuja na kikundi cha wenzake wawili au watatu huku amevalia nguo za kijeshi na vitisho kibao, kwanini uje unitishie? kawa yawezekana wanunue maduka ya wanajeshi wenzao au huko kambini na si kuja kuleta ubabe mtaani.

Mfano kaja na subaru yake kanunua spare, anaenda anafunga kisha baada ya muda anarudi kama mbogo akidai umempa kitu sio kizuri, na haji kwa maelezo mazuri bali ubabe na kikundi cha wenzake.

Kama ulikuja kiraia basi urudi kiraia tuyazungumze, ubabe hausaidii kitu na si kila mtu anakubbali kuonewa kirahisi rahisi.
 
Kamripoti kwa mkuu wake wa kazi achukuliwe hatua za kinidhamu.

Ujeshi wake ni huko kambini na sio kwenye biashara za watu.

Kariri jina lake na namba yake ya usajili. Kama unaweza rekodi mazungumzo yote.

Jeshi halifugi wahuni na majambazi, ATAONDOKA ARUDI KWAO akafanye ubabe kwa mama ake.

Niko nasoma zile REGULATIONS zao hapa, haziruhusu UHUNI na UTOTO.

THE NATIONAL DEFENSE ACT, and THE NATIONAL DEFENSE REGULATIONS.
 
Mimi binafsi naona ni ushamba na ubabe wa kizamani wa baadhi ya wanajeshi, mtu anakuja ofisini kwako kavaa kiraia.
Mnafanya biashara vizuri, Ikitokea biashara imeenda kinyume siku akija kueleza matatizo anakuja na kikundi cha wenzake wawili au watatu huku amevalia nguo za kijeshi na vitisho kibao, kwanini uje unitishie? kawa yawezekana wanunue maduka ya wanajeshi wenzao au huko kambini na si kuja kuleta ubabe mtaani.

mfano kaja na subaru yake kanunua spare, anaenda anafunga kisha baada ya muda anarudi kama mbogo akidai umempa kitu sio kizuri, na haji kwa maelezo mazuri bali ubabe na kikundi cha wenzake. kama ulikuja kiraia basi urudu kiraia tuyazungumze, ubabe hausaidii kitu na si kila mtu anakubbali kuonewa kirahisi rahisi.
Acha utapeli ww kwnn uuze spare mbovu na ushajua kua mbovu ttzo mnapenda kuwaonea raia

Mm hili jambo limenikuta juzi tu jamaa kaniuzia mipira mibovu ila nikamrudishia we unauziwa mpira una kiraka na mwengine tyr ushatoboka aaahhh mnazingua wauza vifaa vya magari
 
Wale jamaa ukiwauzia kitu kizuri huwa wanaambiana wanakuja kundi kama wanafunzi kununua. Ila hakikisha unawauzia mali nzuri hivyo hivyo hata kama unawapiga bei kubwa.
Hata mimi namshangaa sana mleta mada. Wanajeshi ni wateja wazuri sana kulinganisha na raia. Ukiwapa mali nzuri wanaweza kuja kambi nzima kununua kwako. Na hata kama kuna tatizo hutoa nafasi ya kujieleza. Kimsingi jeshi bado ni taasisi inayoaminika.
 
Mimi binafsi naona ni ushamba na ubabe wa kizamani wa baadhi ya wanajeshi, mtu anakuja ofisini kwako kavaa kiraia.
Mnafanya biashara vizuri, Ikitokea biashara imeenda kinyume siku akija kueleza matatizo anakuja na kikundi cha wenzake wawili au watatu huku amevalia nguo za kijeshi na vitisho kibao, kwanini uje unitishie? kawa yawezekana wanunue maduka ya wanajeshi wenzao au huko kambini na si kuja kuleta ubabe mtaani.

mfano kaja na subaru yake kanunua spare, anaenda anafunga kisha baada ya muda anarudi kama mbogo akidai umempa kitu sio kizuri, na haji kwa maelezo mazuri bali ubabe na kikundi cha wenzake. kama ulikuja kiraia basi urudu kiraia tuyazungumze, ubabe hausaidii kitu na si kila mtu anakubbali kuonewa kirahisi rahisi.
kama ccm wanatumia vitisho vya kila wanapo taka kuzuia kushindwa wakitumia jeshi ndio matokeo haya
 
Huo ujasiri wanapata coz wakati wao wanalinda mipaka ,wanasiasa walipaswa kulinda rasilimali za nchi lakini matokeo yake na wao wanasikia kuhusu mikataba mibovu,rushwa ,ubadhirifu Kila siku hivyo kujiona wanajitoa mhanga bure kulinda nchi Yao kama ndani wezi wanafanya wajisikiavyo!wanapata ujasiri huo was kibabe na wanasiasa hawana Cha kuwaambia coz na wao Wana makandokando!!

Viongozi wakiwa smart na wao watakua smart na sio kama ilivyo sasa!
 
Kamripoti kwa mkuu wake wa kazi achukuliwe hatua za kinidhamu.

Ujeshi wake ni huko kambini na sio kwenye biashara za watu.

Kariri jina lake na namba yake ya usajili. Kama unaweza rekodi mazungumzo yote.

Jeshi halifugi wahuni na majambazi, ATAONDOKA ARUDI KWAO akafanye ubabe kwa mama ake.

Niko nasoma zile REGULATIONS zao hapa, haziruhusu UHUNI na UTOTO.

THE NATIONAL DEFENSE ACT, and THE NATIONAL DEFENSE REGULATIONS.
We bichwa Baki na hogo huko 😂😂 Hizo no zake unakariri kutoka kwenye nini? Name tag tu sikuhizi wanavaa kwa kuvizia.
 
Mimi binafsi naona ni ubabe wa usiofaa wa baadhi ya wanajeshi, mtu anakuja ofisini kwako kavaa kiraia...
Mbona hujamalizia stori yako? Kwahio uligoma kumbadilishia au ulikuwa mpole?
 
Back
Top Bottom