Nashauri Wizara ya Utalii waanzishe utalii wa chini ya bahari

TheDreamer Thebeliever

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2018
Posts
2,490
Reaction score
3,584
Habari wadau!

Ni muda sasa wizara zikajitathimini na kuwa wabunifu ili kumsaidia mama kuongeza mapato.

Nilikuwa nashauri serikali kupitia wizara husika kuangalia uwezekano wa kuanzisha utalii watu tukawe tunaenda kutalii chini kabisa ya bahari deep sea bila shaka kutakuwa na utamu wake maana binafsi nimechoka kila siku kuangalia simba wa mbugani.

Nilipata kusoma kwamba chini ya bahari kuna wanyama na samaki pia kuna viumbe ambao waweza kuishi milele very interesting kama kutakuwa na program ya utalii wa chini ya bahari kwenye kina kirefu huko.

Wizara wanaweza kuangalia pia kama wanaweza kuanzisha jumba la makumbusho na masalia ya wanyama wa bahari likajengwa chini ya bahari au kutengeneza tunnel kubwa ya vioo na hotel za chini ya bahari.

Dunia sasa imeenda mbali watu wanaenda kutalii nje ya sayari yetu, sisi bado tupo kwenye utalii wa mbugani basi tujaribu hata wa chini ya bahari na baharini.

Hii itawezesha kuongeza ajira kwa vijana wetu wanaosomea marine, fishing na aquatic science na kada nyingine kama tutaweza jenga mradi kama huu.

Bila shaka wanandoa wengi watapenda kufanya honey moon zao chini ya bahari. Nafikiri hautagharimu pesa nyingi sana.
 
Safi mkuu kwa kuja na mada nzuri mimi ninaiafiki,na nami ningependa kuongeza kitu kingine kwenye mada hii ingawa ni tofauti kidogo,ni msafiri wa mara kwa mara na safari zote lazima nipite pale Mikumi National Park,kinachonishangaza hakuna mwenekano wa wanyama kama zamani,hawa wanyama wamekwenda wapi?yaani miaka ile unaweza una almost all top five but now hakuna kabisa,ni nyani tu,kidogo swala au twiga kuna mwenye kunisaidia hapa?
 
Hata hili wanyama bado sana
Ukiangali Kruger National park walivyo na upinufu wa hali ya juu na kuingiza kipato kikubwa na sio kukaa kwenye Land Rover na kuzunguka kama umepotea [emoji23]

Ushauri wa baharini ni kupata wawekezaji tu na kuwa na sehemu yao kama Egypt vile
 
Mkuu hiyo unazunguka kwenye Land Rover Kama umepotea umetisha Sana mkuu
 
Kuna jamaa alikuwa anaitwa Ali Nacha..., unamfahamu ?

Sasa kama Hoteli tu za nchi kavu zinatushinda na nyingine mpaka zinakuwa Hosteli za wanafunzi unaweza hoteli chini ya bahari na ma-tunnels ya vioo ?

Tuwekeze kwanza nguvu zetu kwenye hizi Serengeti n.k. (known and famous worldwide) kuliko kupeleka visenti vyetu kwenye hizi new mega projects...

ila mtu akitaka deep sea diving nadhani zipo

Habari wadau!

Ni muda sasa wizara zikajitathimini na kuwa wabunifu ili kumsaidia mama kuongeza mapato.

Nilikuwa nashauri serikali kupitia wizara husika kuangalia uwezekano wa kuanzisha utalii watu tukawe tunaenda kutalii chini kabisa ya bahari deep sea bila shaka kutakuwa na utamu wake maana binafsi nimechoka kila siku kuangalia simba wa mbugani.

Nilipata kusoma kwamba chini ya bahari kuna wanyama na samaki pia kuna viumbe ambao waweza kuishi milele very interesting kama kutakuwa na program ya utalii wa chini ya bahari kwenye kina kirefu huko.

Wizara wanaweza kuangalia pia kama wanaweza kuanzisha jumba la makumbusho na masalia ya wanyama wa bahari likajengwa chini ya bahari au kutengeneza tunnel kubwa ya vioo na hotel za chini ya bahari.

Dunia sasa imeenda mbali watu wanaenda kutalii nje ya sayari yetu, sisi bado tupo kwenye utalii wa mbugani basi tujaribu hata wa chini ya bahari na baharini.

Hii itawezesha kuongeza ajira kwa vijana wetu wanaosomea marine, fishing na aquatic science na kada nyingine kama tutaweza jenga mradi kama huu.

Bila shaka wanandoa wengi watapenda kufanya honey moon zao chini ya bahari. Nafikiri hautagharimu pesa nyingi sana.
Ni wazo zuri sana! Tatizo ni uwezo wa ubunifu na kuamua kutoka wizarani sidhani kama watakubali
 
Kuna jamaa alikuwa anaitwa Ali Nacha..., unamfahamu ?

Sasa kama Hoteli tu za nchi kavu zinatushinda na nyingine mpaka zinakuwa Hosteli za wanafunzi unaweza hoteli chini ya bahari na ma-tunnels ya vioo ?

Tuwekeze kwanza nguvu zetu kwenye hizi Serengeti n.k. (known and famous worldwide) kuliko kupeleka visenti vyetu kwenye hizi new mega projects...

ila mtu akitaka deep sea diving nadhani zipo

Tunatakiwa tu dance with music ,twende dunia inapoenda ss km wengi wanaokuja kutalii ni wale wale tu wa miaka yote hatutengenezi watalii wapya sababu utalii wetu unaenda kupitwa na wakati wazungu wamezichukua simba na twiga zetu wamefungua zoo zao huko.
 
Back
Top Bottom