Nashindwa kumfundisha mwanangu jinsi ya kujikinga na unyanyasaji wa kingono

Nashindwa kumfundisha mwanangu jinsi ya kujikinga na unyanyasaji wa kingono

ndandawamalenja

JF-Expert Member
Joined
Nov 1, 2012
Posts
548
Reaction score
664
Kuna tukio la kusikitisha lilitokea mtaani kwangu. Kijana wa form five alikuwa anamlawiti mdogo wake wa kike wa darasa la sita (Mtoto wa mama yake mdogo anayelelewa na mama wa huyo kijana).

Inaonekana hicho kitendo kilianza muda mrefu mpaka siku mama yao (Mama mkubwa wa kabinti) alipogundua kuwa hako kabinti hakawezi kukaa, muda wote kamesimama au kanajilaza, hata wakati wa kula.

Alipokauliza kakasema kana kidonda sehemu ya haja kubwa. Huyo mama alivomkagua akakuta sehemu ya haja kubwa yote ni vidonda, ina maana lile li kijana linasugua tu kila siku mpaka kote kumekuwa vidonda, na sijui lilikuwa linamtisha nini mtoto wa kike mpaka anaogopa kusema kwa mama yake mkubwa. (Mama wa kijana).

Najua kuna mavijana mengi mtaani kwangu kama hayo. Lakini nashindwa jinsi ya kumfundisha kijana wangu (umri miaka 8) jinsi ya kujikinga na miwatu kama hiyo, kwa sababu naichukia naweza hata kuua mimi.
 
Dawa ni kuwa muwazi tu, sisi tukiwa wadogo mzee wetu alikua anatukalisha chini na kutueleza uhalisia wa ulawiti kwa watoto wa kiume. Enzi hizo vitendo havikua vingi sana ila bado alitupa tips za kuepuka. Mfano kukataa zawadi kwa mtu usiyemjua, kuzoeana na vijana wakubwa kiumri na wavuta bangi, kuepuka kukaa nje baada ya saa 12, alinipiga marufuku kuwa karibu na madereva teksi na hata shuleni aliniweka wazi hayo mambo yanatokea boarding schools.

Uwazi ule ulinisaidia sana kuwa alert dhidi ya mambo hayo ila kuyaficha kwa sababu ya aibu ndio inawaacha watoto kuwa vulnerable.
 
Anza na kumwambia mtu yeyote hatakiwi kumgusa, kumchungulia sehemu zake za kukojolea/ za haja/ za siri.. na siku akijaribiwa hata kwa vitisho aje kutoa taarifa.
Na pia Mzazi punguza ukali, ili mtoto asije kukuogopa. Hata akipatwa na kitu anaona jau kukwambia
Pia sali.. kwa imani yako..
 
Tatizo siku hizi mnawaacha watoto muda wote na makatuni tu hamtengi muda wa kuzungumza nao, enzi zetu tulikuwa na muda wa wazazi kutueleza mawili matatu na muda wa kufuatilia katuni TVZ na TVT pamoja na hadithi za Cheichei Shangazi RTD lakini siku hizi ni kuwaharibu tu watoto. Jitahidi uwe na kanuni ya kuwa na muda hata wa kumuhadithia mawili matatu mtoto kabla ya kulala na kumuuliza mambo anayokutana nayo shuleni na mitaani utamjenga vizuri kimaadili na kisaikolojia.
 
Hapo ni kukaa na watoto wako chini uwafundishe namna Gani wanapaswa kuwa makini
 
1. Kuwa karibu sana na mwanao ili asiogope kukuambia chochote.

2. Mfundishe kuhusu sehemu zake za siri. Unaweza kutumia maneno mepesi kama 'kikojoleo', 'kalio' nk na umueleze kwamba hakuna mtu yeyote anaruhusiwa kuzishika bila wewe kuwepo.

3. Mueleze kwamba hakuna mtu mzima yeyote anaruhusiwa kumuomba atunze siri, mbaya zaidi siri inayowaficha wazazi wake.

4. Mueleze kwamba haruhusiwi kuongozana na mtu mzima yeyote yule bila ruhusa yako. Kama ni shule basi amjulishe mwalimu.

Muelekeze haya kwa upole na kwa kumfundisha taratibu usije ukamtisha akawa anaishi kwa hofu. Piga naye stori tu.
 
Kama una nyumba hakikisha unazungushia fance. Na epuka watoto kuzoeana na watu hasa majirani. Acha kukaribisha ndugu ndani kwako. Utaishi kwa amani.
 
Nilidhani nina dhambi nyingi sana, kumbe mimi ni malaika 🙆🏾‍♂️
 
Usione so sema nae kwa lugha ya kitoto. Kuna wimbo fulani wa kuimba na watoto unahusu haya mambo.

Mjengee mtoto kujieleza na kujiamini, study zinaonesha victims wana hali/tabia fulani in common, wengi wamelelewa kwa uoga na vitisho hence self esteem yao iko chini.

kama inawezekana wazazi waishi na watoto wao, kwa case ya extended family usiruhusu watoto walale na watu wazima.


Dunia ina watu wicked nani amefuatilia story ya mwanamke anaitwa Aziza kibibi.
 
Ny*g* ni mbaya sana hasa kipindi cha Balehe me nafikiri kuna haja ya kuruhusu uwazi kwa vijana zaidi kati ya mzazi na watoto ili kueneza elimu zaidi
 
Ukitaka kufanikiwa hakikisha kwanza unaanza kujenga ukaribu nae mfanye kuwa rafiki yako ili yy awe huru kuzungumza na wewe
Kwasababu kiasili watoto wa kike huwapenda sana baba zao
 
Back
Top Bottom