Nipo kweli mahusiano almost two years sasa!
Sema kweli huyu binti nampenda lakini tabia zake hazifai kuwa mke hata kwa kubahatisha!
Kasoro zake!
- Mtu wa visirani na visasi yaani akimchukia mtu hata ukimpatanisha hataki amani tena na mtu huyo!
- Asilimia 95% ya ubongo wake unategemea watu watamwambia nini kuhusu yeye ndio afanye maamuzi hata kama hayana manufaa kwake!
- Hana akili yeyote ya maisha (kuzaa 0 brain ni 89%)
- Ni mpagani kwa asilimia [emoji817]
- Kwenye família yake ni nadra sana mtu kuolewa wengi ni single mothers
- Hajui maneno ya faraja hasa siku ukiwa na stress anachojali yeye ni kumpa ile attention kwa asilimia [emoji817] usipompa atanuna gafla!
- Ni mgumu kuelewa pia ni mgumu kuomba msamaha!
- Sio mtanzania kwahiyo kupoteza damu yangu inawezekana kwa asilimia 50%
Mazuri yake!
- Haniombi pesa hadi nimpe mwenyewe!
- Anaweza kuwa ni muaminifu kwa asilimia 22%{simuamini mwanamke kizembe}
- Sio mvivu anafanya kazi za nyumbani kwa bidii hapendi vitu vikae hovyo!
- Miaka yake ni 20+na kilometres hazijaenda sana kivile japo ni used
- Amekubalia na life style yangu sababu mimi sio mtu wa outing yaani ni mpare fulani aliyekamilika kweli
- Sio single mother
Sema kweli mwanzo kabisa nilimuahidi ndoa ila kwa tabia zake moyo umekosa amani sana hasa napojaribu kufikiria ndoa nakosa usingizi, naogopa kumpotezea muda, naogopa kumpoteza, naogopa kumuoa, naogopa kumuumiza! Nipo njia panda wakuu kumpenda bado nampenda tena sana ila kumuoa ndio siwezi maana dalili za kuingia kwenye majuto ni asilimia [emoji817] Je? Nitamwacha vipi aende?