mafutamingi
JF-Expert Member
- Feb 14, 2011
- 2,773
- 2,183
Nimekuwa nikitumia mtandao was Vodacom tangu mwaka 2000 na kwa ujumla nimekuwa nikiridhishwa na huduma. Lakini katika siku za karibuni nimeanza kutilia shaka huduma zake, hususan vifurushi vyao.
Nasema kwa sababu siku hizi nikinunua kifurushi cha sh 2,500 kinachonipa dk 150 za kutumia wiki nzima, baada ya siku 2 au 3 na nikiwa nimepiga simu chache mara ujumbe kuwa kifurushi kimekwisha.
Jambo hili limekuwa likijitokeza mara kwa mara. Mwanzoni nilidhani ni nahati mbaya lakini naanza kupata shaka kwamba naibiwa, tena mchana kweupe. Swali kwa wale wanaotumia mtandao huu, je wapo ambao wanaoibiwa kama mimi?