Nashindwa kuwaelewa Vodacom

Nashindwa kuwaelewa Vodacom

mafutamingi

JF-Expert Member
Joined
Feb 14, 2011
Posts
2,773
Reaction score
2,183
Nimekuwa nikitumia mtandao was Vodacom tangu mwaka 2000 na kwa ujumla nimekuwa nikiridhishwa na huduma. Lakini katika siku za karibuni nimeanza kutilia shaka huduma zake, hususan vifurushi vyao.

Nasema kwa sababu siku hizi nikinunua kifurushi cha sh 2,500 kinachonipa dk 150 za kutumia wiki nzima, baada ya siku 2 au 3 na nikiwa nimepiga simu chache mara ujumbe kuwa kifurushi kimekwisha.

Jambo hili limekuwa likijitokeza mara kwa mara. Mwanzoni nilidhani ni nahati mbaya lakini naanza kupata shaka kwamba naibiwa, tena mchana kweupe. Swali kwa wale wanaotumia mtandao huu, je wapo ambao wanaoibiwa kama mimi?
 
Ujinga wa hivi vifurushi vya voda na kutoa dakika chache sana za kwenda mitandao mingine tofauti na hapo awali/mitandao mingine.

Kwa mfano,kifurushi cha wiki cha sh 2000(ofa maalumu) wanakupa dakika 150 za voda kwenda voda na dakika 15 tu za mitandao mingine. Hivyo, usipokuwa makini, unaweza kujikuta unazimaliza hizo dakika 15 ndani ya Siku moja au mbili wakati umenunua kifurushi cha wiki cha shilingi 2000 na ukilalamika watakwambia vigezo na mashariti vimezingatiwa.

Kifurushi hiki kina nafuu kwenye kutoa MB tu ambapo wanakupa GB moja utumie ndani ya hizo siku 7.
 
Utawaelewa tu, endelea kuchangia hasara ya 5.09 Billions ya mwaka jana
 
Ujinga wa hivi vifurushi vya voda na kutoa dakika chache sana za kwenda mitandao mingine tofauti na hapo awali/mitandao mingine.

Kwa mfano,kifurushi cha wiki cha sh 2000(ofa maalumu) wanakupa dakika 150 za voda kwenda voda na dakika 15 tu za mitandao mingine. Hivyo, usipokuwa makini, unaweza kujikuta unazimaliza hizo dakika 15 ndani ya Siku moja au mbili wakati umenunua kifurushi cha wiki cha shilingi 2000 na ukilalamika watakwambia vigezo na mashariti vimezingatiwa.

Kifurushi hiki kina nafuu kwenye kutoa MB tu ambapo wanakupa GB moja utumie ndani ya hizo siku 7.
Sasa kimekuwa 3000
 
Jamani mwenzenu sijawahi kuilalamikia mitandao ya simu. Hawa voda wananipigia simu Hadi wanatia huruma Mara watume sms eti ninunue dk 50 mitandao yote kwa sh 700 nitumie siku 7.

Ushenzi wao huu wa kuwaibia wateja nilihama na kuacha line iwe hewani kwa wanaonitafuta tu na si vinginevyo. Sasa kuilalamikia mitandao ya simu ambayo Ina ushindani kibao huu si ustaarabu Mimi Nina record za kuwalalamikia tanesco.
 
Kuna mtu aliwahi kuwapigia akiwalalamikia,akasema km wataendelea kimfanyia huo mtima nyongo,atauhama mtandao;Jamaa wakamjibu kuwa akitaka kuhama asihame peke yake Bali atafute wengine 99 ili wawe 100,Voda jeuri Sana.
 
Hahahaha huyo jamaa hivi still atakuwa kazini kweli? Voda viburi flows
 
Sina hakika km bado Wapo kazini au lah?,Lkn kiujimla wahudumu wa Voda ni jeuri sana na ni full kiburi.
 
Back
Top Bottom