Nashukuru kiuno changu ni 36 tu, hivyo ni miongoni mwa wale ambao sipo hatarini kukumbwa na tatizo lolote

Nashukuru kiuno changu ni 36 tu, hivyo ni miongoni mwa wale ambao sipo hatarini kukumbwa na tatizo lolote

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Posts
60,660
Reaction score
121,325
Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Profesa Mohamed Janabi amesema kuwa iwapo mwanaume mzunguko wa kiuno chake utazidi 40 (inchi) na mwanamke ukizidi 35 kitakuwa ni kiashiria cha matatizo ya kiafya.

Profesa Janabi amesema kuwa iwapo viuno vitazidi inchi hizo ni changamoto, maana yake ana uzito mkubwa ambao unawaweka kwenye hatari ya kupata magonjwa yasiyo ya kuambukiza.

Janabi ameyasema hayo leo Julai 28, 2024 wakati akizungumza na washiriki wa NBC Marathon jijini Dodoma.

Chanzo: mwananchi_official

Haya akina adriz, Arovera, King Kong III, Bujibuji Simba Nyamaume, mrangi na Bila bila Marafiki zangu wenye Viuno kuanzia 43 hadi 49 huu ni wakati sasa wa ama kuvipunguza muwe kama Mimi GENTAMYCINE mwenye 36 au anzeni mapema sana kuandaa Vitanda vyenu pale Wodi za Mwaisela, Sewahaji na Kibasila Muhimbili National Hospital.
 
Hii kauli ya Janabi imenikumbusha Titanic, walisema "hii hata Mungu hawezi kuizamisha", basi haijamaliza hata safari yake ya kwanza.

Janabi ajichunge na kauli yake ya kukufuru, aombe toba kwa Muumba wake.

Yeye aongee faida za kuwa mwembamba lakini asiingize kujilinganisha.

"Mungu hajaribiwi" - wahenga.
 
Back
Top Bottom