Nashukuru Mungu kwa baraka hizi, biashara yangu imekua

BradFord93

JF-Expert Member
Joined
Oct 11, 2017
Posts
917
Reaction score
2,217
Chuo nilimaliza mwaka 2017 pale ruaha Catholic

Kulikuwa na duka home kutokana na uongozi mbaya likafilisika wakalifunga....nilikuwa na laki 5 tu nilipoamua kulifungua upya(nnadhan mnajua kuwa laki 5 ilivyo ngum kuinua duka la reja reja)

Nilikuwa na girlfriend aliniacha baada ya kukosa ajira plus kutokuwa na muelekeo mzuri kimaisha(hili nalo lilinipa hasira vile vile)

Ndipo nilipoamua kujiweka imara zaidi kwenye biashara

Niliingia mtandaon nkasearch kuhusu huduma znazotolewa na maximalipo na selcom(kwa njia ya simu lkn maana sikuwa na mtaji wa mashine)

Nkachagua selcom kwa kuangalia hudum zao plus faida katika vocha....luku na huduma zngne

Sikuishia hapo nkajiunga mobistock(hawa wanahusika na kurusha vocha mitandao yote....hii niliichagua kwa ajili ya huduma za kutolea hela(hii ni njia niliyobuni mwenyew....sikuwa na hela ya kulipia till)...mobistock niliitumia kama till ya tigopesa wakat selcom niliitumia kama till ya mpesa na airtel money

Mwishowe nikajiunga na tigorusha....hawa wana faida nzuri mno kila ununuapo kwa epin pesa

Nikajikaza mno kukuza mtaji wa duka....nilipambana kiasi kwamba mpka faida niliiweka dukan....hakukua na hela yangu bali zot zilikuwa ni za duka....!!

Kadria hela zilipozidi kuongezeka ndipo nilipozidi kuongeza akili ya kuongeza huduma

Nikaongeza huduma za ufundi simu...kusajili laini na kuchajisha simu

Nilipambana juu chini huku nikiweka pemben anasa na mapenzi....!!

Ili kukuza mtaji nkajiunga tala na branch ambao mpk sasa tumeshafika kwenye laki na nusu....hawa nnawawekea akiba kila siku kwa ajili ya kulipia mkopo...!!

Pia nnacheza mchezo wa kuchangishana ambao nnapokea 270k

Yote hayo ni kwa ajili ya maisha na malengo yangu...!!staki kuckia kuhusu mahusiano...!!maana nnajua akili yangu na biashara hii ukiendekeza wanawake....vyote utafeli

Tuombe uzima ndugu zangu...mwezi huu nmeamua kupanga chumba...kila kitu kipo tyr

Maisha yanawezekana kama ukijua ulipotoka....ulipo na unakoenda....madhaifu yako...kipaji chako lakini hasa watu ulonao katka maisha yako

Kwa sasa sijutii kufanya biashara maana nnaona huku ndo nilikotakiw kuwepo ili nifanikiwe

*Pichaza chini kabisa ni kipindi duka linaanza*View attachment 987966View attachment 987968View attachment 987969View attachment 987967

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hongera sana mjasiriamali mwenzangu. Nimepanda ulivyompiganaji kimaisha.

Mimi mwaka 2017 nianzisha duka la reja reja kwa mtaji wa Tsh 1. 5milioni na Mpesa mtaji wa 1milioni. Ninakosa muda wa kujigawa kukaa mwenyewe nimemuajiri muuzaji, wakati naanza mauzo ya duka kwa siku yalikuwa 35 elfu hadi 40 elfu. Ila sasa mauzo yameshuka hadi elfu 8 kwa siku na duka linapungua bidhaa na fedha sioni.

Baada ya kuona vitu vya kupima kama sukari, unga, maharage, ngano,mchele vinanipa hasara nimeamua kuviacha na sasa nauza vinywaji na Mpesa tu ila bado mauzo hayakidhi yanatosheleza kulipia frame tu na kodi TRA, sioni faida kwangu.

Naomba tupeane mbinu na mikakati ya kuboresha biashara hii maana inaumiza kichwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cha kwanza hii biashara ukitaka kufanikiwa...kaa mwenyew...wew nd unayejua uchungu wa hela yako...pia vitu vya kupima ndo vyenye faida km ukivisimamia....wahi kufungua chelewa kufunga ht mpk saa 4 cku...lugha nzuri kwa wateja....kingine mikopo kwa wateja ipungue...!!usikopeshe kila anayekuja kulia shda.....kingine n mahesabu...kuwa n daftari la mahesabu....then mshirikishe Mungu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hapo ukae mwenyewe tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Dah hivi nikikwambia nilipotea kweli utasemaje?

Huwezi amini ila ndiyo kilichotokea. Nipo Mbagala muda huu
Ndvyo palivyo kwetu...ukitaka lbd akufuate stend....ukisema uanze kumfuata kwa maelekezo....utajikuta ushaingia gest na ushapita mapokezi....

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimepotea wakati narudi.
Gari limekuja tupu la G/Mboto Masaki, nikapanda nikakaa nyuma huku nina earphone kumbe linaenda Mbagala.
Nimekuja kushtuka baadae baada ya kuona njia siielewi.
Ndvyo palivyo kwetu...ukitaka lbd akufuate stend....ukisema uanze kumfuata kwa maelekezo....utajikuta ushaingia gest na ushapita mapokezi....

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…