Hongera sana mjasiriamali mwenzangu. Nimepanda ulivyompiganaji kimaisha.
Mimi mwaka 2017 nianzisha duka la reja reja kwa mtaji wa Tsh 1. 5milioni na Mpesa mtaji wa 1milioni. Ninakosa muda wa kujigawa kukaa mwenyewe nimemuajiri muuzaji, wakati naanza mauzo ya duka kwa siku yalikuwa 35 elfu hadi 40 elfu. Ila sasa mauzo yameshuka hadi elfu 8 kwa siku na duka linapungua bidhaa na fedha sioni.
Baada ya kuona vitu vya kupima kama sukari, unga, maharage, ngano,mchele vinanipa hasara nimeamua kuviacha na sasa nauza vinywaji na Mpesa tu ila bado mauzo hayakidhi yanatosheleza kulipia frame tu na kodi TRA, sioni faida kwangu.
Naomba tupeane mbinu na mikakati ya kuboresha biashara hii maana inaumiza kichwa.
Sent using
Jamii Forums mobile app