Nashukuru ninachokipata na ninachopewa

Baba yangu hajafanya makosa
 
Umenikumbusha nilivyokua mdogo, tunafurahia baba akirudi nyumbani na kumkimbilia kumuwaoooo, ilikua best part of our day, I hope kwake naye tulimpa faraja kama watoto.

Familia ni kila kitu 🤍
Bila Shaka na Wewe una watoto
 
Uzi mzuri lakini kitendo cha kumsema vibaya baba hapo ndo amekosea kabisa.
Unajua maana ya makosa ya wazazi (MADINGI)
kukimbia uzao wake
Kuitelekeza familia Yake hili ndio kosa ambalo ninazungumia Mimi.
Na zile kutia mimbo hovyo mabinti halafu huduma mbovu.

Inapendeza sana watoto wengi wawe baba mmoja na mama mmoja.
 
Unajua maana ya makosa ya wazazi (MADINGI)
kukimbia uzao wake
Kuitelekeza familia Yake hili ndio kosa ambalo ninazungumia Mimi.
Na zile kutia mimbo hovyo mabinti halafu huduma mbovu.

Inapendeza sana watoto wengi wawe baba mmoja na mama mmoja.
Kumbe wewe umelelewa na mzazi mmoja? Sikujua mkuu, sorry, basi usingejumlisha wazazi wote.
 
maisha hayana kanuni au mfumo, hivyo vitu vidogo kwa wengine ni vikubwa mno.

nikiwa mwenyewe nipo nipo, ila niki enda nyumbani. Mzuka haswa.
Mara hili au lile.

Money comes and go, but family is everything.
 
Nimekutana na huu uzi umenikumbusha,jana asubuhi ya saa 07:23 AM pale Magomeni Kagera maarufu Oil Com (wanaotumia hii barabara ya Morogoro wanapajua) nilipata sononeko kubwa sana la nafsi nilipomuona mwanaume mwenzangu,baba wa familia na muhangaikaji mwenzangu(umri above 40+) akiiingia Toyota Rav4 kwa mbele na pikipiki yake,yule brother alikuwa amevaa Kaunda Suit ya brown na bag mgongoni yaani yupo tu smart wala siyo bodaboda bodaboda wanajulikana.

Yaani within a second jamaa alikuwa hafai,alikuwa hajavaa helmet kichwa chote damu puani mdomoni masikioni yaani hajiwezi,anabebwa pale yaani dah!kilichonifanya nikamuhurumia sana ni mazingira niliyotoka home,wakati natoka mbio mbio (mimi huwa navaa kofia) nilisahau kuvaa so nikampita mwanangu wa kike aged six alikuwa anakinga maji bombani aingie msalani kuwahi shule,nimetembea kama hatua saba mbele kakaniita ”Baba unaenda kazini?” kabla sijajibu kakaniambia “umesahau kofia” kisha mbio ndani kwa mama yake kakaniletea nikapokea nikavaa kisha kakasema ”bye baba” nikamjibu aaya nikampiga kakofi mgongoni mie mbio.

Nilipoona hili tukio nilivaa viatu vya jamaa kwa hii situation aliyokutana nayo,ameaga vizuri wanae nyumbani kwa furaha akili asubuhi imechangamka mipango yote halafu dah,anakutana na mzinga anaishia hospital au kwingine aisee niliwawaza mkewe na wanae wakisikia kilichompata mpendwa wao ilibaki kidogo nilie,ila ndiyo maisha tumeandikiwa in short vipo vitu tunaishi navyo vinaumiza sana but ndiyo reality lazima vitukute kama kwa kutaka au kutotaka muhimu tuendelee kuombeana heri mke na mume migogoro ya ndani iishe pale mmoja wenu anainua mguu kwenda kutafuta mtakie mema hata likimtokea baya liwe na afadhali.

NB:Aisee mkuu uliyepata ajali jana eneo tajwa hapo juu kama upo humu ikitokea Mungu amekujaalia ukakaa sawa ukikutana na hii post usiache kusema neno kuhusu maendeleo yako,pole sana.
 
Uzi mzuri lakini kitendo cha kumsema vibaya baba hapo ndo amekosea kabisa.
hajamsa baba ila amesema ukweli kabsa wazee wetu mao
wamezngua kwa namna moja au nyingne na ss tujaribu kutokurudia makosa hajakosea
 
Fate mkuu. Sisi tupambane tu hatuijui fate yetu, ila mwamba hapo kuwasema wababa waliotuzaa vibaya nashindwa kuelewa kama anajua aliyokuwa anapitia baba yake......
 
Hakika walisema Kushukuru ni Kuomba tena halafu wazee na maandeko wakaongezea kwamba Usiposhukuru kwa kile kidogo ulichopewa hata ukipewa kikubwa hutoshukuru.
 
Fate mkuu. Sisi tupambane tu hatuijui fate yetu, ila mwamba hapo kuwasema wababa waliotuzaa vibaya nashindwa kuelewa kama anajua aliyokuwa anapitia baba yake......
Bila Shaka umeelewa nilichomaanisha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…