Nimekutana na huu uzi umenikumbusha,jana asubuhi ya saa 07:23 AM pale Magomeni Kagera maarufu Oil Com (wanaotumia hii barabara ya Morogoro wanapajua) nilipata sononeko kubwa sana la nafsi nilipomuona mwanaume mwenzangu,baba wa familia na muhangaikaji mwenzangu(umri above 40) akiiingia Toyota Rav4 kwa mbele na pikipiki yake,yule brother alikuwa amevaa Kaunda Suit ya brown na bag mgongoni yaani yupo tu smart.
Yaani within a second jamaa alikuwa hafai,alikuwa hajavaa helmet kichwa chote damu puani mdomoni masikioni yaani hajiwezi,anabebwa pale yaani dah!kilichonifanya nikamuhurumia sana ni mazingira niliyotoka home,wakati natoka mbio mbio (mimi huwa navaa kofia) nilisahau kuvaa so nikampita mwanangu wa kike aged six alikuwa anakinga maji bombani aingie msalani kuwahi shule,nimetembea kama hatua saba mbele kakaniita ”Baba unaenda kazini?” kabla sijajibu kakaniambia “umesahau kofia” kisha mbio ndani kwa mama yake kakaniletea nikapokea nikavaa kisha kakasema ”bye baba” nikamjibu aaya nikampiga kakofi mgongoni mie mbio.
Nilipoona hili tukio nilivaa viatu vya jamaa kwa hii situation aliyokutana nayo,ameaga vizuri wanae nyumbani kwa furaha akili asubuhi imechangamka mipango yote halafu dah,anakutana na mzinga anaishia hospital au kwingine aisee niliwawaza mkewe na wanae wakisikia kilichompata mpendwa wao ilibaki kidogo nilie,ila ndiyo maisha tumeandikiwa in short vipo vitu tunaishi navyo vinaumiza sana but ndiyo reality lazima vitukute kama kwa kutaka au kutotaka muhimu tuendelee kuombeana heri mke na mume migogoro ya ndani iishe pale mmoja wenu anainua mguu kwenda kutafuta mtakie mema hata likimtokea baya liwe na afadhali.
NB:Aisee mkuu uliyepata ajali jana eneo tajwa hapo juu kama upo humu ikitokea Mungu amekujaalia ukakaa sawa ukikutana na hii post usiache kusema neno kuhusu maendeleo yako,pole sana.