Nashukuru ninachokipata na ninachopewa

Nashukuru ninachokipata na ninachopewa

Familia kama familia; paradiso ndogo, sehemu ya amani na makubaliano na waswahili walisema mchuma janga hula na wa kwao. Kwa vyovyote iwavyo mta'solve' na kusonga mbele kama familia ikiwa mmoja wenu amepotoka.

👆👆Nina experience na hilo

Lakini kinyume chake ni sehemu hatari sana ikiwa viongozi wa hio taasisi hawachukuliani mizigo. Namwona mhanga mkubwa ni mwanaume, hatusikii mwanaume kuonewa ndani ya familia lakini mwanamke anaon............
 
Well said bro. Furaha ipo katika vitu vidogo sana tunavyochukulia for granted.

Daima huwa napata faraja fulani nikirudi nyumbani na kukuta shangwe la kupokelewa na watoto, kupewa kesi zao za siku nzima na kukumbishiwa ahadi ya zawadi ulizotoa.

Kwa watoto wetu sisi ni kila kitu kwao. Huwa wanahisi baba anaweza fanya chochote kile, na hiyo inaleta hisia ya thamani kubwa katika mioyo yetu.

Nathamini sana ule usemi wa "chizi akiwa kazini, nyumbani ni baba".
Familia inatia Nguvu kwenye utafutaji
 
Maisha ya zamani matamu sana ,familia ni muhimu ila kwa Sasa naona huruma unakuta mzazi mmoja Yuko mkoa mwingine na mwingine sehemu nyingine kisa kazi.

Familia Zinaleta furaha hata kama ni masikini.
 
Salute kwa mabro wanaokusapoti kiuchumi sio , Basi sawa
Sometimes inakuwa hivyo brother.Nipo Dar es salaam.Bado nausoma mji.

Mji huu unataka akili nyingi na sio Nguvu.Mana watu hawalali na watu hawaliziki na walichonacho hasa Kwa Sisi wageni.Lazima tufanye kila njia ili mkono uende kinywani pasipo kuvunja sheria za NCHI YETU TANZANIA 🇹🇿
 
Maisha ya zamani matamu sana ,familia ni muhimu ila kwa Sasa naona huruma unakuta mzazi mmoja Yuko mkoa mwingine na mwingine sehemu nyingine kisa kazi.

Familia Zinaleta furaha hata kama ni masikini.
Kweli kabisa brother
 
Back
Top Bottom