Kagame ameongea vizuri sana, Hata Nyerere amewahi kulizungumza hili vizuri sana jinsi Wabelgiji na Wajerumani walivyogawana utawala wa Ufalme wa kale wa Rwanda. Sehemu moja ikabaki Kongo, hiyo ndo inayokaliwa na Wanyamulenge, na sehemu nyingine ikabaki Rwanda. Nyerere akasema kuwa ni makosa makubwa kwa nchi za Kiafrika za leo zilizorithi ardhi husika kutaka hizo ardhi lakini watu waliokuwemo katika ardhi hizo haziwataki. Yaani haiwezekani nchi ya Kongo ya leo kuitaka ardhi ambayo wanyamulenge wanaishi lakini haiwataki wanyamulenge.