Nashukuru sana Uongozi wa JamiiForum kwa kunitambua kama Moja ya wanachama wenye mchango kwa mwaka 2024

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
28,297
Reaction score
68,017
NASHUKURU SANA UONGOZI WA JAMIIFORUMS KWA KUNITAMBUA KAMA MOJA YA WANACHAMA WENYE MCHANGO KWA MWAKA 2024.

Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli

Hii kwangu niite heshima ya pekee. Kutambulika na kutambuliwa ni jambo kubwa ambalo wanadamu wengi hulipenda na kulitafuta.

Mimi kama Taikon nimefurahi sana Kuona kile ninachokifanya kumbe kinaonekana kwa watu wengine. Zaidi kile ninachokifanya kinabadilisha maisha ya watu wengine na kuwafanya kuwa watu Bora wenye tija kwenye jamii yetu.

Taarifa hii wala nisingeipata au ningeipata kwa kuchelewa sana kama asingenitafuta Moja ha member humu akinipa pongezi ya kushinda Tuzo.

Niseme machache;

1. Kwangu Jamiiforum ni jukwaa la kutoa maoni, mafundisho, na fikra zangu ambazo naona zitasaidia watu Free in charge.
Kwani napenda watu waishi maisha ya furaha, amani na uhuru.

2. Kwangu Jamiiforum ni kama nyumbani. Sio rahisi siku ipite bila kuingia humu JF.
Nimejiunga JF tangu mwaka 2011 sambamba na Facebook ingawaje kwa akaunti nyingine hii ni kusema JF ninamiaka zaidi ya 12.

3. Kwangu JF ni chanzo cha taarifa. Mimi sio mtazamaji na mpenzi wa kuangalia Luninga, video. Napenda maandishi kuliko picha na video. Ndio maana navutiwa na JF kwa habari za mtandao wa hapa nchini.

4. Kwangu JF ni kisima cha kuchotea Maarifa.

Humu ninauzoefu wa miaka 12 kwa kusoma nyuzi za Wakulungwa mbalimbali, kaka na dada walionitangulia. Nikiri kusema Moja ya platform zilizonijenga kifikra ni pamoja na JF ukiachilia mbali hobby na interest za kupenda kujisomea vitabu na kufikiria mambo pekeangu.

5. Kwangu JF ni kijiwe cha kuja kupiga Soga, kuleta mzaha, kutaniana na kusumbuana na baadhi ya memba.
Napenda utani, masiakhara na kucheza na Akili za watu😊. Hii kwa wale wajanja wanaonijua wananipuuza😂😂. Napenda kucheza na Akili za watu wanaochukulia mambo serious, watu wanaochelewa kuelewa mambo.

6. Kwangu JF ni sehemu ya kukusanya taarifa, kuijua jamii halisi inayotumia uhusika bandia.

7. Kwangu JF ni uwanja wa burudani.
Kuna mambo yanayonifanya niburudike hasa nikikutana na ligi za watu mbalimbali humu. Napenda sana Ligi
😅. Sipendi nikutana na mtu anayetaka yaishe kirahisi. Ligi kwangu ni burudani lakini ndio sehemu ambayo watu wengi huonyesha uhalisia wao kwani wanakuwa wanakasirika kwelikweli.

Pia napenda Riwaya na stori ziwe na uongo au kweli kwangu sio shida kwani kwenye stori Kuna mambo mengi ukiacha Ukweli au utunzi wa simulizi yenyewe. Kwetu waandishi huwezi kuwa mwandishi mzuri bila kusoma stori au Riwaya mbalimbali bila kujali ubora wa Riwaya au stori hizo.

Mwisho nampongeza Maxence Melo na UONGOZI mzima kwa kutuletea Mtandao huu hapa nchini. Sisi tunajua umuhimu wake na tutautumia umuhimu huo vilivyo.

Pia nakupongeza Maxence Melo kwa kutambua nafasi za Members waliopo humu jukwaani. Kuwatambua na kuwapa zawadi ni Moja ha kiashiria kuwa unazidi kukua na unafanikiwa.

Members wote wanamchango kwa namna Moja ama nyingine. Kila mtu uwepo wake hapa ni muhimu.
Hivyo Zawadi, Tuzo au utambuzi wowote kwa baadhi ya members wachache isiwe huzuni, kikwazo, Maumivu au chanzo cha mtu yeyote kujihisi vibaya. Kwani lengo la Tuzo ni kufurahia uwepo wetu Kila mmoja hapa ndani. Hivyo tuendelee kuishi kama zamani.

Hata hivyo ingefaa Angalau kwa mwaka kuwe na JF day Angalau mara moja kwa mwaka ambapo wanaJF wote tutakutana ili tufurahie na tubadilishane mawazo. Hakutakuwa na haja ya kutambuana kwa mafekeo(I'd bandia). Hii kuna mdau alishawahi kuwasilisha hapa.

Soma Pia: Wanachama wa JamiiForums waliotambuliwa kwa kuwa na michango chanya Jukwaani kwa mwaka 2024

Msije sema nimeandika mambo mengi kisa nimetambuliwa 😅😅 maana Kuna zile njemba zangu nazijua nazo zinajijua jinsi zinavyonichukulia na kuniona.

Watibeli ni watu wa amani na UPENDO siku zote.

Acha nipumzike Sasa.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa Sasa Dar es salaam
 
NASHUKURU SANA UONGOZI WA JAMIIFORUMS KWA KUNITAMBUA KAMA MOJA YA WANACHAMA WENYE MCHANGO KWA MWAKA 2024.

Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli

Hii kwangu niite heshima ya pekee. Kutambulika na kutambuliwa ni jambo kubwa ambalo wanadamu wengi hulipenda na kulitafuta.
Mimi kama Taikon nimefurahi sana Kuona kile ninachokifanya kumbe kinaonekana kwa watu wengine. Zaidi kile ninachokifanya kinabadilisha maisha ya watu wengine na kuwafanya kuwa watu Bora wenye tija kwenye jamii yetu.

Taarifa hii wala nisingeipata au ningeipata kwa kuchelewa sana kama asingenitafuta Moja ha member humu akinipa pongezi ya kushinda Tuzo.

Niseme machache;

1. Kwangu Jamiiforum ni jukwaa la kutoa maoni, mafundisho, na fikra zangu ambazo naona zitasaidia watu Free in charge.
Kwani napenda watu waishi maisha ya furaha, amani na uhuru.

2. Kwangu Jamiiforum ni kama nyumbani. Sio rahisi siku ipite bila kuingia humu JF.
Nimejiunga JF tangu mwaka 2011 sambamba na Facebook ingawaje kwa akaunti nyingine hii ni kusema JF ninamiaka zaidi ya 12.

3. Kwangu JF ni chanzo cha taarifa. Mimi sio mtazamaji na mpenzi wa kuangalia Luninga, video. Napenda maandishi kuliko picha na video. Ndio maana navutiwa na JF kwa habari za mtandao wa hapa nchini.

4. Kwangu JF ni kisima cha kuchotea Maarifa.
Humu ninauzoefu wa miaka 12 kwa kusoma nyuzi za Wakulungwa mbalimbali, kaka na dada walionitangulia. Nikiri kusema Moja ya platform zilizonijenga kifikra ni pamoja na JF ukiachilia mbali hobby na interest za kupenda kujisomea vitabu na kufikiria mambo pekeangu.

5. Kwangu JF ni kijiwe cha kuja kupiga Soga, kuleta mzaha, kutaniana na kusumbuana na baadhi ya memba.
Napenda utani, masiakhara na kucheza na Akili za watu😊. Hii kwa wale wajanja wanaonijua wananipuuza😂😂. Napenda kucheza na Akili za watu wanaochukulia mambo serious, watu wanaochelewa kuelewa mambo.

6. Kwangu JF ni sehemu ya kukusanya taarifa, kuijua jamii halisi inayotumia uhusika bandia.

7. Kwangu JF ni uwanja wa burudani.
Kuna mambo yanayonifanya niburudike hasa nikikutana na ligi za watu mbalimbali humu. Napenda sana Ligi😅. Sipendi nikutana na mtu anayetaka yaishe kirahisi. Ligi kwangu ni burudani lakini ndio sehemu ambayo watu wengi huonyesha uhalisia wao kwani wanakuwa wanakasirika kwelikweli.
Pia napenda Riwaya na stori ziwe na uongo au kweli kwangu sio shida kwani kwenye stori Kuna mambo mengi ukiacha Ukweli au utunzi wa simulizi yenyewe.
Kwetu waandishi huwezi kuwa mwandishi mzuri bila kusoma stori au Riwaya mbalimbali bila kujali ubora wa Riwaya au stori hizo.

Mwisho nampongeza Maxence Melo na UONGOZI mzima kwa kutuletea Mtandao huu hapa nchini. Sisi tunajua umuhimu wake na tutautumia umuhimu huo vilivyo.
Pia nakupongeza Maxence Melo kwa kutambua nafasi za Members waliopo humu jukwaani. Kuwatambua na kuwapa zawadi ni Moja ha kiashiria kuwa unazidi kukua na unafanikiwa.

Members wote wanamchango kwa namna Moja ama nyingine. Kila mtu uwepo wake hapa ni muhimu.
Hivyo Zawadi, Tuzo au utambuzi wowote kwa baadhi ya members wachache isiwe huzuni, kikwazo, Maumivu au chanzo cha mtu yeyote kujihisi vibaya. Kwani lengo la Tuzo ni kufurahia uwepo wetu Kila mmoja hapa ndani. Hivyo tuendelee kuishi kama zamani.

Hata hivyo ingefaa Angalau kwa mwaka kuwe na JF day Angalau mara moja kwa mwaka ambapo wanaJF wote tutakutana ili tufurahie na tubadilishane mawazo. Hakutakuwa na haja ya kutambuana kwa mafekeo(I'd bandia). Hii kuna mdau alishawahi kuwasilisha hapa.

Msije sema nimeandika mambo mengi kisa nimetambuliwa 😅😅 maana Kuna zile njemba zangu nazijua nazo zinajijua jinsi zinavyonichukulia na kuniona.

Watibeli ni watu wa amani na UPENDO siku zote.

Acha nipumzike Sasa.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa Sasa Dar es salaam
Hiyo JF Day naafiki mawazo Yako ingawa Nina mashaka kwa Usalama wetu hasa wakosoaji wa.....Salama?
 
Back
Top Bottom