Nashukuruni kwa kuja kunipa Kampani. Ila ndugu zanguni kwa aliyejisahau akaondoka na Iphone 11 Pro Max yangu namuomba

Nashukuruni kwa kuja kunipa Kampani. Ila ndugu zanguni kwa aliyejisahau akaondoka na Iphone 11 Pro Max yangu namuomba

Bill Lugano

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2018
Posts
1,189
Reaction score
6,450
Nisiwe mchoyo wa fadhila kwa upendo ambao ndugu zangu wawili wa JF waliamua kushiriki nami weekend iliyoisha jana. Kwa kweli jamaa walifurahi na kufurahia.

Wengi walishangaa mzee alipoamua kuwafanyia tour wakaliona lile jumba analoishi kupitia skype. Jamaa walidhani ni Ikulu nilipata shida sana kuwahikikishia kuwa siyo ikulu ni mansion tu ya mzee.

Wengi waliondoka wakiamini baba yangu ni rais au alikuwa rais wa nchi flani akafanya ufisadi.nmesikitika hawataki kuamini kuwa pale siyo ikulu ni home.

Anyway... watu walikula na nliwaruhusu wabebe walivyotaka. Tatizo nadhani katika kubeba kuna ambaye alichanganya bahati mbaya akabeba na simu moja wapo kati ya ninazotumia IPHONE 11 PRO MAX. Leo ndio nmegundua kuwa sinayo maana huwa nabadilisha badilisha simu.

Shida yangu ni moja tu nataka nimpe huyo mtu password afungue simu kisha atume some documents kwangu then simu abaki nayo tu. Najua alibeba pasipo kujua siwezi mwambia arudishe.

Mimi kuna vitu mtu akitoka navyo home huwa havirudi tena maana hata laptop yangu kuna mlinzi siku moja alijisahau akaiona pale kibarazani nimeicha akaichukua ili anitunzie akasahau akaenda nayo kwao.

Siku tatu nikagundua moja ya laptops zangu haipo nilipo itrace nikaiona kwake na picha zake zikatumwa kwangu nilimwambia tu alete nitoe documents zangu then atumie laptop hakujua aifanyie nini laptop ya mil 6.9 tsh.

Anyway sikutaka kumfanya ajisikie vibaya nlii flash tu nikampa akatumie akaenda kuuza laki 7. Nlimshangaa maana maskini hakujua hata bei yake akamuuzia mhindi mmoja.

Yule mhindi ilibidi anitafute baada ya kupeleka kwa mtaalamu wake wa IT ili naye awe huru kuitumia maana kuna vitu hakuweza ku access basi nikamwelekeza akaendelea kutumia yule mlinzi nlimwona ameuza kwa bei ya chini sana nikamwongeza 700,000 Nyingine anunue boda boda kwa zile pesa imsaidie.

So hata hii Iphone aliyejisahau akachukua nitamwachia tu ila inabidi awasiliane nami bila hivyo haitamfaa kitu ina security kubwa sana. Na kama akitaka kuuza naweza mtafutia wateja wa ukweli.

Jamani nashukuru ingawa hamkuja wengi but wengine waliwakilisha JF. Sisi sote ni ndugu tutendeane wema. Naangalia tu movie kwenye hii screen kubwa 72 inch 3D. Karibuni sana mnitembelee.... maana hii inapendeza mkiwa wengi kama mpo theatre hivi.

Asanteni na Mbarikiwe sana.
 
Anyway... watu walikula na nliwaruhusu wabebe walivyotaka. Tatizo nadhani katika kubeba kuna ambaye alichanganya bahati mbaya akabeba na simu moja wapo kti ya ninazo tumia IPHONE 11 PRO MAX. leo ndo nmegundua kuwa sinayo maana huwa nabadilisha badilisha simu.

Shida yangu ni moja tu nataka nimpe huyo mtu password afungue simu kisha atume some documents kwangu then simu abaki nayo tu.
Sijui uliechukua iphone umeelewa
 
We dogo tumbavu sana yaani ukiwa na stress ukiona tu post ya bwana mdogo ukaisoma bas stress tupa kule. [emoji16][emoji16]

Eti ukamuongezea mlinzi laki 7 plus na zile laki 7 alizouza laptop inakua m 1.4 kiasi ambacho huwezi pata bodaboda labda used
 
Sifahamu bei ya boda boda.but nlidhani ni tsh milion 1. Mi sifahamu kwa kweli bei ya boda boda.but si angesema?mbona alishukuru tu?angesema.

We dogo tumbavu sana yaani ukiwa na stress ukiona tu post ya bwana mdogo ukaisoma bas stress tupa kule. [emoji16][emoji16]

Eti ukamuongezea mlinzi laki 7 plus na zile laki 7 alizouza laptop inakua m 1.4 kiasi ambacho huwezi pata bodaboda labda used
 
Back
Top Bottom