Ok let me close this case now;-
1. Diamond kwa hatua aliyofikia sasa Ruge hana ubavu wa kumuangusha, nakubali Ruge ni 'jiniaz' ndio wa hii sekta ila amechelewa sana kudeal na Diamond coz ana fanbase kubwa mno kwenye mpira tunaita 'die hard fans' ambao wako tayari kumsapoti kwa lolote, ni rahisi kuwaangusha wasanii kama kina Nandy,Ruby ila sio rahisi/haiwezekani kumdondosha msanii mwenye hazina ya mashabiki kama Diamond. Huyu Diamond namfananisha na timu nnayoishabikia kule majuu 'Manchester United', ni timu ambayo imepitia katika kipindi kigumu kirefu kutokana na kuondoka kwa kocha wa muda mrefu SAF aliyeweza kuitengeneza vizuri hiyo timu, lakini pamoja na kushindwa kufanya vizuri kisoka still zinapotajwa timu zinazoingiza mkwanja mrefu ni lazima uitaje, viwanja vinajaa kama kawaida, na kwenye usajili wanamwaga mpunga wa kutosha huku wachezaji wakilipwa mishahara minono, hiki kiburi cha kufanya hivyo ni kutokana na msingi waliokwisha ujenga kwa mda mrefu 'fanbase' inayoendelea kuwapatia mapato ya kutosha hata wanapotetereka kisoka. Sasa huo ndio mtaji mkubwa alionao Diamond na WCB kwa ujumla.
2. Teknolojia,....Ruge na CMG waliweza kuwashika vilivyo wasanii wa bongo enzi hizo kwavile hawakuwa na alternative, kwa maana kama hausikiki redioni tena 'Redio pendwa' ndio basi tena kifo chako cha muziki kimefika. Dunia imebadilika, vijana waliokuwa wanasubiria XXL kusikiliza nyimbo mpya wengi wamehamia Instagram/You Tube, wimbo ukipigwa XXL tayari wanakuwa wameshaucheki You Tube ama wameudownload kwenye blogs, hawana muda wa kusubiri B 12 autambulishe na kuwaaminisha kwamba wimbo ni mzuri, wanajudge wenyewe kulingana na utashi wao, hili limethibitishwa kwenye uzinduzi wa wimbo wa AliKiba 'Mvumo wa Radi', pamoja na kutaka kuwaaminisha watu kuwa huo wimbo ni mkali sana ila watu wameukataa na umebuma[emoji16][emoji16][emoji16], hii ni one of the biggest disappointment CMG kuwahi kuipata, walijiaminisha kila wanachoamua kiwe juu lazima kiwe lakini kumbe sahivi watz wajanja sio wa enzi zile za kina Dudubaya[emoji23][emoji23][emoji23].
3. Mimi naamini WCB wataendelea kufanya vizuri, na kufanya kwao vizuri hakutaifanya CMG kupotea, wale jamaa wako vizuri kimkakati, na wenyewe wataendelea kulishika soko la entertainment tz japo ule 'umungumtu' wao hautakuwa kama zamani kutokana na upinzani wa media nyingine na nguvu ya mitandao. Kwasasa mitandao inanguvu sana asikwambie mtu kiasi kwamba imekuwa tishio kwa hawa wamiliki wa redio, ndio maana baada ya kugundua hilo kwa sasa karibu kila redio ina channel U Tube, account za Insta/Twitter ili kukabiliana na ushindani wa sasa.
CASE CLOSED!!!![emoji13]