Nasikia kwenye kupambana na foleni Round about ni nzuri kuliko mataa ya barabarani ni kweli?

Nasikia kwenye kupambana na foleni Round about ni nzuri kuliko mataa ya barabarani ni kweli?

Lycaon pictus

JF-Expert Member
Joined
Jan 31, 2021
Posts
9,189
Reaction score
16,128
Nimesikia ikisemwa kuwa round about ni nzuri kupambana na foleni sababu magari yanakuwa kwenye mwendo muda wote. wataalamu, Hili lina ukweli wowote?
 
Hilo jambo lina ukweli kwa 100%.
Mataa yawekwe mahali ambapo haiwezekani kuweka round about (kwenye ufinyu wa eneo tu) au kwenye madereva wakorofi wasiopenda kuheshimu sheria bila shuruti.

Yote kwa yote, Roundabout haihitaji uwepo wa umeme wa Tanesco, haina gharama wala kero.
 
Round about ni nzuri sababu gari hazisimami zinakuwa kwenye mzunguko sawa. Hata njia ya mbagala haikuwa na foleni sababu ya round about nyingi
 
Roundabout zinafaa kwenye sehemu zisizo na magari mengi....
 
Ila roundabout napo kunataka umakini na ustaarabu wa madereva
Kwenye kuruhusu nani apite kwa kila wakati
Au napo roundabout atakuwepo traffic police

Ova
 
Ila roundabout napo kunataka umakini na ustaarabu wa madereva
Kwenye kuruhusu nani apite kwa kila wakati
Au napo roundabout atakuwepo traffic police

Ova
Kweli. Hilo linahitaji ustaarabu. Lakini pia kuna sheria nani apite kwanza.
 
Mfano hai roundabout ya Msamvu Moro town inayogawa barabara kuu tatu hakunaga foleni ya kindezi siku wakilogwa kuweka traffic lights kutakua na foleni ya kufamtu
Kweli kabisa pale siku wakiweka mataa ndio mwanzo wa foleni morogoro
 
Back
Top Bottom