mkuu mleta mada usijitoe ufahamu kwani inajulikana kabisa hao waliofungua kesi kina said na wenzake wawili walikuwa viongozi huko zanzibar chini ya mbowe..huyo Said yeye alikuwa makamu mwenyekiti zanzibar kwa miaka 15 miaka yote hiyo wanapokea ruzuku,wanafanya vikao na mikutano,wanalipana posho na mishahara,wanapanga mipango na shughuli za chama n.k..lakini ajabu baada ya mbowe kushindwa uchaguzi kwa Lissu na timu yake kushika hatamu ndani ya mwezi wakafungua kesi kudai eti zanzibar wanapunjwa kwenye mgao na rasilimali za chama yaani washasahau kwamba wao ndio walikuwa viongozi kwa miaka 15 huko zanzibar..sasa hujiulizi miaka 15 wapo ofisini wana maamuzi yote na wanapaga mipango na bajeti hawakuona kama wanapunjwa na wala hawakudai mgao wa mali wala rasilimali miaka yote 15 mkiwa viongozi.! badala yake mgao wa mali na rasilimali uje kuwadai kina Lissu na heche walio na mwezi mmoja ofisini .a sio wao waliokaa miaka 15 ofisini huku wakiwa na power ya kujipa watakacho..na kwanini hiyo kesi wafungue wao viongozi wa zamani walioshindwa uchaguzi na hata kama wakipewa huo mgao wa mali wanaotaka je, wanapewa wao waliofungua kesi au watapewa ofisi ya chama zanzibar ambayo ina viongozi wapya na wala hawajalalamika kupunjwa au kudai chochote toka makao makuu maana hawa walio ofisini sasa ndio wenye haki ya kudai mapunjo kwani chadema zanzibar hakijawatuma wao kudai haya wanayodai..kuhusu wazo lako kwa Chadema wangekubali mgao wa mali mapema labda kwa sababu haijawa wazi baada ya hizo mali za chama na rasilimali kugawiwa je,zinachukuliwa na nani je,wanapewa taasisi Chadema zanzibar au wanapewa binafsi hao waliofungua kesi.? vp kama wanataka huo mgao wapewe binafsi badala ya chama zanzibar..Chadema HQ hawawezi kukubali mali za chama kumilikishwa watu binafsi walioshindwa uchaguzi na walio ofisini sasa watumie nini? kwako ww yote hayo huyaoni
miaka 15 ofisini msijigawie hizo rasilimali alafu mnakuja kuwadai wenye mwezi mmoja ofisini si kukomoana tu hapo