Rais John Pombe Magufuli ametoa msimamo wa taifa kuhusiana na maambukizi ya Corona pamoja na chanjo inayopigiwa kampeni na dunia kwamba kila nchi lazima ipatiwe chanjo hiyo.
Watanzania wengi wamemuelewa Rais na wanachukua tahadhari na pia wameelewa msimamo wa Rais kuhusu chanjo ya Corona. Ila penye wa kuelewa na wakupinga hawakosekani, na kuna watanzania wengi haswa wenye itikadi tofauti za kisiasa wanampinga Rais tena wakitumia nguvu kubwa sana kuhamasisha watu wakachanjwe.
Mimi binafsi nina maswali machache kuhusu hiyo chanjo:
1. Imetumika wapi kama majaribio na matokeo yake ni yapi hadi tuje kuchomwa huku kwetu? Tusisahau mwaka Jana walisema kabisa chanjo ingepatikana ilitakiwa ianzie kutumika Africa wakatoa sababu eti kuna uhaba wa health facilities kwa hiyo kukinga ni bora kuliko kutibu, sasa wameona ngoma imegoma na waafrika hawajaathirika kwa kiasi kikubwa walivyotaka bado wanalazimisha, kulikoni?
2. Wakati UK wanareport wastani wa vifo 1000 kwa siku, USA wao wana wastani wa vifo 4000 kwa siku. Kwanini wasitoe hiyo chanjo kwenye hizi nchi zilizoathirika zaidi ili kuonyesha effectiveness ya chanjo na kutokomeza vifo kabla ya kuja Africa?
3. Wataalamu wa mfumo wa upumuaji wanasema hakuna chanjo inayoweza kupambana na virus vya mfumo wa upumuaji kwa 100%, wanasema kama kuna chanjo inaweza kuwa effective 50% 60% ila kikubwa wanachoshauri ni wanadamu kubadili mfumo wa maisha ikiwa ni pamoja na Kula, kunywa na kubadili tabia zinazoweza kuchochea maambukizi. Je, kwanini WHO hawatumii nguvu kubwa kutoa hii hamasa kwa dunia kama wanavyohamasisha chanjo?
4. Tumsikilize Mtanzania mwenzetu hapa chini na tutafakari huu upendo mkubwa hivi kwa mataifa yaliyoendelea wa kutaka kutulinda ili tusife wakati wao wanakufa kila siku tena kwa maelfu unasababishwa na nini?
Your browser is not able to display this video.
I STAND WITH MY PRESIDENT JOHN POMBE MAGUFULI[emoji106][emoji123]
Mi umeniambia, ngoja nichanganye na zangu ntaleta mlejesho. Ila mabeberu Mungu anawaona. Na safari hii yuko upande wetu ,tuendelee kuchukua tahadhari na taratibu za kiafya tunazoshauriwa.
Unaweza kuwa na hoja ya msingi kwenye hili, ila nilitegemea busara na uchambuzi wa kisayansi zaidi kama Nchi kwenye kupinga hii chanjo, tupende tusipende hili gonjwa lipo na linaua, suala la kutulazimisha sisi huku Africa tuchanjwe haliwezi kuepukika maana muingiliano baina ya Nchi na Nchi ni mkubwa sana, haitakuwa na maana wao wachanjwe halafu sisi tubaki kama tulivyo.
Nikija kwenye hii hoja kwamba wanataka kutumaliza, hoja kama hii haiajaanza leo, ilianza kipindi gonjwa la ukimwi lilipochachamaa, lakini kwa busara zao hao wanaotaka kutumaliza, wametuletea ARVs ambazo kwa kiasi kikubwa zimesaidia kutubakisha hai, leo iweje kwenye COVID 19 ndio watumalize?
Nikija kwenya malaria, hawa jamaa wametulete vyandarua, wametoa billions of money kwa ajili ya kampeni za kutokomeza malaria, japo inafahamika vyanzo vya mazalia ya mbu ni uchafu, kwanini kama kweli tuna shaka na tiba zao tusionyeshe hata mifano ya sisi kujikinga ili wasituingilie?
Africa ilipofikia kwa sasa, hakuna namna tutaruka maamuzi ya hawa jamaa, watakachotaka tutafanya, tupende tusipende.
Ukifuatilia sana hii ishu mfano pale Uingereza selikali iliingia kwenye mgogoro na kampuni inayotengeneza hii chanjo kwa madai ni kwa usalama wa taifa.
Baadae umoja wa Ulaya wakasema mazungumzo yanafanyika.
Mpaka sasa hivi haieleweki ni usalama upi uliosababisha huo mgongano.
Kuna ukoo nawajua huwa hawakubali chanjo yoyote. Wazee wao wananiambia walizaliwa miaka ya 1940s na wao hawajawahi pewa chanjo wala watoto wao, wala wajukuu, wala vitukuu. Sio chanjo ya ndui sijui surua wala TB.
Ukiangalia vizuri sio unaweza ukatamani kufanya uchunguzi zaidi sababu upo ukweli kwamba waliochanjwa chanjo ya TB bado wanaugua TB na wapo wasiochanjwa na hawaugui
Tusikubali chanjo kama fashion, tuhoji na kujiridhisha kwamba hizo chanjo zina faida au hasara na tuchague mbadala kama upo.
Kila kukicha mzungu hufikiri afanye nini apate Mali za bule kutoka Africa, Mwafrica Naye kila kukicha hufikiri ni kwa namna Ipi aweze kuomba cha kumsaidia Kutoka Kwa mzungu.
Mzungu anapotengeneza Jambo lake, Africa ijiandae kulikubali Kwa lazima, na hata asiyeumwa atameza tu dawa nakwambia!
Unaweza kuwa na hoja ya msingi kwenye hili, ila nilitegemea busara na uchambuzi wa kisayansi zaidi kama Nchi kwenye kupinga hii chanjo, tupende tusipende hili gonjwa lipo na linaua, suala la kutulazimisha sisi huku Africa tuchanjwe haliwezi kuepukika maana muingiliano baina ya Nchi na Nchi ni mkubwa sana, haitakuwa na maana wao wachanjwe halafu sisi tubaki kama tulivyo.
Nikija kwenye hii hoja kwamba wanataka kutumaliza, hoja kama hii haiajaanza leo, ilianza kipindi gonjwa la ukimwi lilipochachamaa, lakini kwa busara zao hao wanaotaka kutumaliza, wametuletea ARVs ambazo kwa kiasi kikubwa zimesaidia kutubakisha hai, leo iweje kwenye COVID 19 ndio watumalize?
Nikija kwenya malaria, hawa jamaa wametulete vyandarua, wametoa billions of money kwa ajili ya kampeni za kutokomeza malaria, japo inafahamika vyanzo vya mazalia ya mbu ni uchafu, kwanini kama kweli tuna shaka na tiba zao tusionyeshe hata mifano ya sisi kujikinga ili wasituingilie?
Africa ilipofikia kwa sasa, hakuna namna tutaruka maamuzi ya hawa jamaa, watakachotaka tutafanya, tupende tusipende.
Wameanzia mbali sana hawa, tangu kwenye ukimwi, kutuletea mbegu za kisasa za mazao na kuua mbegu zetu za asili, kuhamasisha mapenzi na mahusiano ya jinsia moja ili tusizaliane, ila bado Mungu anatupigania