Nasimamia Vipi Biashara ya chakula bila Uwepo Wangu?

Uso wa nyoka

JF-Expert Member
Joined
Mar 17, 2014
Posts
4,791
Reaction score
2,375
Wakuu Mimi ni mgeni hapa katika jukwaa lakini nimekuwa nikipita humu kwa muda mrefu bila kujiunga.
Kutokana na kuona michango ya wanajamii mlio wengi, nimegundua humu kuna watu wengi wanaoweza kutoa ushauri wenye hekima na unaoweza kumsaidia mtu.
Nisiwachoshe kwa maelezo marefu, ni kwamba nimefungua biashara ya kuuza supu, mtori na chakula cha mchana kwenye Bar moja. Makubaliano na mwenye Bar ni kumlipa kila mwezi kwa utaratibu wa sh. 6000 kwa siku.
Nimeajiri watumishi 2 ambao wanapika na kuhudumia wateja, tatizo ni kwamba nalazimika kuwepo wakati wote ili kusimamia mauzo wakati nina shughuli zangu nyingine zinazohitaji niwepo huko.
Sasa swali ni, je naweza kuisimamia vipi biashara hii bila uwepo wangu bila kusumbuliwa na mauzo? Mkumbuke hawa watu wanatakiwa kulipwa hata kama watakuwa hawafanyi kazi inavyostahili, bado wataniangalia mimi ifikapo mwisho wa mwezi.
Natumaini maelezo yangu yanaeleweka na mtanisaidia kwa hili. Karibuni!
 
  • Kwa kuwepo kwenye manunuzi ya vyakula na kujua kila manunuzi yakiisha roughly unaingiza kiasi gani.
  • Kwa kujua kawaida ya mauzo ya hapo kila siku, siku gani mauzo ni makubwa na siku gani mauzo madogo, na average ya mauzo mazuri siku mbaya na nzuri
  • Kupenda kushitukiza ukipata muda kupita na kuangalia au marafiki ndugu / kupita hapo na kuchunguza

Hizo zote hapo juu zitakuwa ni indicators mambo yakienda tofauti na ulivyozoea chunguza / dadisi ni kwanini (utaona kwamba itabidi siku za mwanzo itabidi uwepo hata kwa mwezi mmoja au zaidi ili uone hali inavyokwenda, hata kama sio wewe kama wife ni sharp itabidi akae hapo.

Mwisho wa siku ni wewe kupata faida (kwahio hata kama unaibiwa kidogo, lakini bado unapata faida sio mbaya), sababu kumbuka ni bora wewe kutumia 5% ya muda wako na kupata faida ya 1%, kuliko 100% ya muda wako hata kama utapata faida ya 100% (Time is Money)
 

Nashukuru sana Mkuu, Nitaufanyia kazi ushauri wako.
 
Ushauri mzuri sana, mimi nadhani biashara yoyote hutakiwi kumwachia sana mfanyakazi hadi wewe mwenyewe hujui hata mapato kwa siku ni kiasi gani, tafuta likizo kaa hapo walau hata wiki na uone inaendaje ndio umkabidhi mtu. Pia kila weekend kaa wewe au mkeo ili kama kuna mchezo unafanywa utashangaa siku hiyo yanayofunguka. Ninakumbuka mdogoangu alinialika twende kwenye farm yangu ukaone kuku, nikajua ni suala la masaa tuondoke. Kufika naona anawatuma kupeleka mayai na dreva kwa wakala watarudi jioni. Siku hiyo tuliokota mayai idadi mara mbili ya waliyokuwa wanampa hesabu wakisingizia kuku wengine miezi 5 bado hawajaanza. Tulishangaa kupokea wateja wanaotaka mayai wakati yeye hauzi rejareja, yaani nilijifunza kitu. Kwa hiyo kuanzia siku hiyo ilibidi iwekwe record mpya ya utagaji bila hivyo angeendelea na hiyo ya zamani. Kila wiki unapaswa kupitia biashara yako. Mimi nikiishaona biashara sintaweza kuifuatilia vizuri hata kama inaonekana ina faida kiasi gani sifanyi kabisa.
 
Mimi nikiishaona biashara sintaweza kuifuatilia vizuri hata kama inaonekana ina faida kiasi gani sifanyi kabisa.

Ni kweli unayosema lakini mara nyingine asilimia ndogo ya kingi ni bora, kuliko asilimia mia moja ya sifuri (kisichokuwepo). Ninachomaanisha hapa ni zile biashara ambazo mtu unamkodisha biashara yako aiendeshe na wewe kukupa kiasi fulani kwa siku (hata kama unajua yeye anaingiza kingi kiasi gani na wewe anakupa kidogo unavumilia).

Au hata kama unajua unaibiwa (ili mradi bado faida ipo na inazidi matumizi) unaweza ukavumilia. Sababu Tanzania ya sasa kila mahali ni kuchakachua, watu sio waaminifu kabisa.
 
ni kweli usemayo ila inategemea umeiweka hiyo faida kwa kiwango gani, wengi wetu tunategemea walau tupate 90% ya tulichowekeza sasa kama biashara inakuwa 50% labda uwe nazo nyingi au bora ufanye franchise nipate tu asilimia Fulani kama cocacola vile nisipoteze muda wangu kabisa hapo, kitu ambacho startuo business zetu hazijafika huko.
 

Unachozungumza ni kweli, tatizo ni shughuli tulizonazo wengine ni nyingi na kipato cha kawaida, sasa unajaribu kugawanya vyanzo vya mapato ili upate kidogo huku na huku sasa ndio tunashindwa kuwepo sehemu zote kwa wakati mmoja.
Itabidi nijitengenezee likizo kwa kweli.
 
Ni kweli shtukiza siku moja hata kwa sick leave unafika kuanzia asubuhi unawaambia leo tuko pamoja. Kama kuna ujinga hawawezi rudia maana hawajui lini unaweza kuja kukaa hapo tena.
 
Kama wadau wengine walivyosema kuwepo ni muhimu kwa siku za kwanza na wakati fulani biashara ikisha changanya ili upate record zote. La msingi hapa ni supervision km umeoa mke hana kazi ni mahali pake akasimamie km wote mnakazi zingine basi maelezo ya kwanza ni yafaa. Ila pamoja nakufuatilia unatakiwa uwawekee kiwango cha chini kukupa ww baada ya kulipa kwa mwenye baa kwa wastani kila siku km utaona sasa huwezi kabisa kusimamia. Lazima wafanye kazi kwa target fulani hapo watachangamka.

Sent from my BlackBerry 9790 using JamiiForums
 
mi ninashauri kama alivyosema mjumbe ,uistudy hiyo biashara yako kwa muda kusudi ujue mauzo kwa siku,siku mbaya,na siku zingine baada ya hapo uwawekee watumishi wako mauzo kwa siku kuwa kiasi fulani,kwa hiyo wewe unakua na hesabu ya wiki,let the bzs run itself!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…