Uso wa nyoka
JF-Expert Member
- Mar 17, 2014
- 4,791
- 2,375
Wakuu Mimi ni mgeni hapa katika jukwaa lakini nimekuwa nikipita humu kwa muda mrefu bila kujiunga.
Kutokana na kuona michango ya wanajamii mlio wengi, nimegundua humu kuna watu wengi wanaoweza kutoa ushauri wenye hekima na unaoweza kumsaidia mtu.
Nisiwachoshe kwa maelezo marefu, ni kwamba nimefungua biashara ya kuuza supu, mtori na chakula cha mchana kwenye Bar moja. Makubaliano na mwenye Bar ni kumlipa kila mwezi kwa utaratibu wa sh. 6000 kwa siku.
Nimeajiri watumishi 2 ambao wanapika na kuhudumia wateja, tatizo ni kwamba nalazimika kuwepo wakati wote ili kusimamia mauzo wakati nina shughuli zangu nyingine zinazohitaji niwepo huko.
Sasa swali ni, je naweza kuisimamia vipi biashara hii bila uwepo wangu bila kusumbuliwa na mauzo? Mkumbuke hawa watu wanatakiwa kulipwa hata kama watakuwa hawafanyi kazi inavyostahili, bado wataniangalia mimi ifikapo mwisho wa mwezi.
Natumaini maelezo yangu yanaeleweka na mtanisaidia kwa hili. Karibuni!