Fidel80
JF-Expert Member
- May 3, 2008
- 21,947
- 4,470
hehehehehehe
Unacheka nini toa thanks basi mpaka aongee anae ng'ata usiku?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
hehehehehehe
Mshindi wao kwa mwaka huu kwa majaji alikuwa ni Kelvin Mbati!!!! Naona aibu ilkuwa kubwa kama wangethubutu kutompa Paschal Casian. Iwe fundisho kwao baada ya kumchaga Misoji mwaka jana bila ridhaa ya Watanzania. Mwaka jana yule dogo ambaye alikuwa ni composor ana alikuwa anacheza gitaa yaani yule mshindi wa pili ndiye alitakiwa awe mshindi
nakubaliana nawe....haya ni majungu tu, mwanzaoni ni hawahawa waliokua wanaiponda, sasa wameumbuka baada ya onesho kung'ara , swala la upendeleo kama wangetaka wangedanganya tu......kwani nani alikua akimonitor kura za wananchi, ni wao wenyewe kamati ya BSS, WALIHISI KUNA WATU WANGEPIKA MANENO WAKAWAKATA KILIMILIMI.Haya ni majungu, acheni hizo Ritha toka mwazo alisha jua Kevin sio mshindi. Kwa walio fuatilia watakua wanaua kabisa kuwa ila siku baada ya show waliku wanaoneysha idadi ya kura , hakuna siku hata moja Kevin akaonekana ana kura nyingi ,sasa iweje eti Kevin aandaliwe wakati matokeo ya Kura tulikua tuna yaona kila siku?
Halafu ile sio show ya Ritha kama yake pekee ,ile ina wadhamini wakubwa kama VOdacom na TBL , wote hao sio wajinga kumuachia Ritha ajiamulie anavyotaka sababu eti yeye ni exective producer.
Watu wengi ni wa kwanza kulalamika wakati ukiwauliza kama walivote utakuta hakuna hata mmoja aliye vote .
Kuhusu suala la Misoji Nkwabi kwamba alipewa, Kwanza kabisa Misoji ali perfrm bonge la nyimbo " I will always love u" na kuiimba vizuri sana kiasi cha watu wote kumkubali, na pia, kura zote zilikua zinaoneyshwa na mara zote Misoji alikua anaongoza,
Naomba muwe na uhakika na manacho sema.
You are not sure, haikuwahi hata siku moja kuonyeshwa idadi ya kura kwa BSS ya mwaka jana, tell us something else.
Kweli Fidel,unajua A.Y amezaliwa na bahati sana lakini mi najua huyu jamaa ni supa star with under ground qualities,kuna vitu vingi vya kisupa staa jamaa anamiss pamoja na kusafiri sana lakini swaga zake awapo on stage mi huwa bored!!!Majaji walitumia siku ile kuhitimisha au ni mapenzi binafsi ya nyie watazamaji mkaja na matokeo yenu ukimbini kuwa Pascal ndo mshindi.
Nilishangaa supa staa AY alivyo panda jukwaani alitegemea atashangiliwa watu ziiiiiiiiiiii wanamwangalia tu dah kila akijaribu kukonga nyoyo za watu lakini wapi.
Bamutu mie simo,nilichosikia ni kuwa kunamtu alitakiwa kupewa endapo zisingetiliwa maanani kura za mashabiki,kuhusu Kelvin mi sijui,ila kwanini wote wamzungumzie yeye,au ndio hapendwi na wote?acheni majungu jamani nakubaliana kabisa na mtoto wa kishua hoja zake ya kuwa wengi hampigi kura mmekalia kupika majungu mwanzo mwisho... kila mmoja wetu alijua anachukua cassian sasa mambo ya kevin kuandaliwa yametoka wapi??? kura zenyewe hazikuonyesha kuwa alikuwa na chnace hata ya kuwa wa pili jamani. mngesema peter msechu sawa ila sio kevin.... ushindi ulienda kwa haki na hakukuwa na upendeleo wowotw acheni majungu jamani hayajengi
Kwa mtu kama mimi,hata kama nipo Dar,huwezi niambia nimpigie kura mtu dhaifu na asiye na uwezo kama Mbati eti kisa tuu anatoka mkoa mmoja na mimi,wewe hata siku ya pambano la Kaseba na Cheka bila shaka ungeniambia nimshabikie Kaseba kisa tuu katokea Dar!!Kuna kitu kimejitokeza kwenye ushindi wa huyu dogo ambacho watu wengi hawakukiona, kura ndio zimembeba na si uwezo. Tofauti na miaka mingine shindano hili mwaka huu lilipata umaarufu sana mikoani hasa mikoa iliyokuwa na wawakilishi. Ukilinganisha dar na mwanza kwa mfano ambapo mashindano ya bongo star search yanaangaliwa na watu wengi mwanza zaidi ya dar, hii inatokana na ukweli kwamba kwa dar watu wana option ya kuangalia american idol, so u think u can dance na takataka nyingine nyingi(mbishi aende DSTV aulize idadi ya wateja wa dar na mwanza) hivyo hawashoboki na BSS kihivyo hata wakiangalia. Kingine watu wa mikoani ni likely kupiga kura kuliko hapa dar, kwanza kwa kuwa mikoani watu wanajiona wapo karibu na mshiriki kuliko dar hivyo kumpigia kura mshiriki wa mkoa wao ni rahisi zaidi ya dar. pia kuna ka element ka dar against mikoani ambapo mikoa yote inaungana kuashindana na dar linapokuja suala la kushindana, kwao ni bora mshindi atoke mkoa mwingine wowote kulikoni dar.
Hivi vigezo vya kura vitatosha kumfanya mtu kama pascal awe star kweli?
Tetesi nilizozipata hivi karibuni ni kwamba baadhi ya majaji wa bongo star search wameujutia uamuzi wao wa kukubali kuwa kura za mashabiki ndio zitakuwa muamuzi wa mwisho,na si maamuzi ya majaji,ukweli ni kwamba kwenye kabinet ya majaji kulikuwa na baadhi yao waliopenda ile tuzo iende kwa mtu ambaye walikuwa wameshamuandaa,lakini endapo maamuzi ya majaji yangechukua nafasi naamini kabisa pale diamond pasingekalika,poleni sana majaji na sera zenu za ukandamizaji,naomba hizi sera za kura zidumishwe hadi kwenye ma miss.Mwisho nampongeza sana bwana Pascal Cassian kwa kuibuka mshindi wa haki!!!