KERO Responded Nasotea Leseni baada ya kuhitimu VETA Mbeya, tatizo ni VETA, Jeshi la Polisi (Traffic HQ) au mfumo wa pamoja unaotumika?

KERO Responded Nasotea Leseni baada ya kuhitimu VETA Mbeya, tatizo ni VETA, Jeshi la Polisi (Traffic HQ) au mfumo wa pamoja unaotumika?

  • Thread starter Thread starter Anonymous
  • Start date Start date
Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Mimi ni miongoni mwa wanafunzi tuliomaliza mafunzo ya udereva katika Chuo cha VETA Mbeya mwezi Septemba 2025, Baada ya kumaliza mafunzo, tuliambiwa hatuwezi kupata leseni ya udereva Daraja E bila kwanza kufanya mtihani wa Jeshi la Polisi (Traffic HQ).

Tulifanya mtihani huo tarehe 19 Desemba 2025 na nikafaulu. Hata hivyo, tangu hapo nimekuwa nikizunguka katika ofisi mbalimbali za Polisi kufuatilia leseni yangu bila mafanikio.

Nilifika katika ofisi za Polisi mikoa ya Tanga, Pwani (Kibaha) na Njombe Machi 2026, lakini niliambiwa matokeo yangu hayaonekani kwenye mfumo. Baadaye nilikwenda Songwe tarehe 28 Mei 2026, ambapo matokeo yangu yalionekana. Hata hivyo, nilielezwa kuwa cheti changu hakijaingizwa kwenye mfumo na nikatakiwa nirudi VETA Mbeya nilikosoma ili waweke taarifa hizo.

Nilifika VETA Mbeya tarehe 22 Juni 2026, lakini nikaambiwa mfumo unasumbua na hadi sasa kila ninapopiga simu naambiwa bado tatizo halijatatuliwa.

Kinachonisikitisha ni kwamba vyuo binafsi vinaonekana kuingiza taarifa za wanafunzi wao kwa wakati, na wahitimu wake hupata leseni bila usumbufu. Sisi tuliomaliza VETA tunaendelea kusubiri kwa miezi mingi bila majibu ya kueleweka.

Naomba mamlaka husika zitoe ufafanuzi:
  • Tatizo lipo kwa VETA, Jeshi la Polisi (Traffic HQ) au mfumo wa pamoja unaotumika?
  • Kama VETA Mbeya imezuiwa au kusitishwa kutoa sifa za Daraja E, wananchi waambiwe wazi ili tusiendelee kupoteza muda na fedha kufuatilia huduma ambayo haipatikani.
  • Ikiwa ni hitilafu ya mfumo, itatuliwe haraka kwa kuwa imewaathiri wahitimu wengi, si mimi peke yangu.
Kwa sasa, imepita zaidi ya miezi tisa tangu nimalize mafunzo, lakini bado sina leseni ya Daraja E, hali inayonikosesha fursa za ajira wakati maisha yangu yanategemea kazi ya udereva.

Naomba mamlaka husika zilifanyie kazi suala hili kwa haraka ili sisi wahitimu wa VETA Mbeya tupate haki yetu ya kupata leseni kwa wakati.

Soma Majibu kutoka VETA:VETA: Tunawasihi wateja wetu kuwa na uvumilifu na kuzingatia taratibu kuhusu vyeti na leseni za Udereva.
 
kwenye hii nchi kwa sasa tambua kuwa mkono mtupu haulambwi...
 
Sio Veta mbeya, Veta karibia zote Mkuu, kasomee vyuo vya polisi.
 
Back
Top Bottom