Nassari aumbuka bungeni...

Mandla Jr.

JF-Expert Member
Joined
Dec 15, 2013
Posts
3,098
Reaction score
631
Mjumbe wa Bunge Maalumu la Katiba, Joshua Nassari, juzi alijikuta akiumbuka bungeni baada
ya kushindwa kutaja kanuni aliyoitumia, kuomba mwongozo.Hali hiyo ilitokea muda mfupi kabla
ya wajumbe kupiga kura za kumchagua Mwenyekiti wa Bunge hilo.

Kuumbuka kwa mjumbe huyo ambaye pia ni Mbunge wa Arumeru Mshariki, kulitokana na Mwenyekiti
wa Muda wa Bunge hilo, Pandu Ameir Kificho, kumtaka kutaja kanuni aliyoitumia.

Hata hivyo, baada ya kusita kwa muda Nassari bila kutaja kanuni aliyoitumia, alisema wajumbe wengi
hawajasikia utaratibu unaotumika katika upigaji kura kwa sababu walichelewa kwenye msongamano wa
watu getini.
 

Haya Tuma salaamu
 
Inategemea uwelewa wangu sikuona tatizo lolote la Mh. J Nassari kuuliza swali bila kusoma kanuni, kwani kanuni zenyewe hazielezi kura niya aina gani. Wazi au siri. Hivyo shangaa kanuni na sio Mh. Nasari.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…