DuaZaMama
JF-Expert Member
- Jun 2, 2025
- 1,882
- 4,153
BODI ya Ligi ya Tanzania (TPLB) imemteua Mwenyekiti wa klabu ya Azam FC, Nassor Idrissa ‘Father’ kukaimu nafasi ya Mwenyekiti wa TPLB ambayo imekuwa wazi kufuatia kujiuzulu kwa aliyekuwa Mwenyekiti Steven Mnguto mnamo Juni 13, 2025.
Aidha nafasi ya Mtendaji Mkuu iliyoachwa wazi kufuatia kusimamishwa kwa Almas Kasongo na Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Wallace Karia sasa imechukuliwa na Ibrahim Mwayela ambaye awali alikuwa Meneja Fedha wa TPLB.
Barua ya TPLB kwenda kwa klabu za Ligi Kuu ambayo imefichuliwa na Mwananchi Digital imesema: “Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) inakujulisha kuwa Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB), Nassor Idrissa amekaimu nafasi ya Mwenyekiti wa Bodi hiyo kwa mujibu wa ibara 33:5 ya Kanuni za Uongozi za TPLB.
“Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) inakujulisha kuwa Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB), Nassor Idrissa amekaimu nafasi ya Mwenyekiti wa Bodi hiyo kwa mujibu wa ibara 33:5 ya Kanuni za Uongozi za TPLB.” imesema barua hiyo.
“Katika hatua nyingine Meneja Fedha wa TPLB, CPA Ibrahim Mwayela ameteuliwa kukaimu nafasi ya Ofisa Mtendaji Mkuu (CEO), baada ya Almasi Kasongo kusimamishwa kazi mwishoni mwa juma lililopita. Bodi inatarajia ushirikiano wa dhati wa klabu yako kwa viongozi hao,”—imesema barua hiyo.