I am baba Ian
New Member
- Sep 2, 2021
- 1
- 1
Mimi ni Mtanzania ambaye niliomba kujiunga na programu ya uzamili (Master’s) katika Chuo cha COSS, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), mwaka 2025, na nikapata nafasi ya kujiunga.
Baadaye, nilielezwa kuwa wanafunzi waliochaguliwa katika programu hiyo walikuwa wachache, hivyo masomo yasingeweza kuanza. Kutokana na hali hiyo, nilishauriwa na ofisi inayoshughulikia masuala ya uzamili kuahirisha masomo yangu hadi mwaka uliofuata.
Mwaka 2026 ulipofika, nilirejea chuoni ili kuendelea na masomo kama nilivyoshauriwa. Hata hivyo, nimekuwa nikikumbana na changamoto na majibu yanayotofautiana. Wakati mwingine naelezwa kuwa nilipaswa kusitisha masomo rasmi (freeze) badala ya kuyaahirisha (postpone); wakati mwingine naelekezwa kwenye ofisi ya udahili, huku nyakati nyingine nikiambiwa kuwa usajili umefungwa na siwezi kuendelea na masomo.
Nilipojaribu kuomba tena kupitia mfumo wa ARIS kama mwombaji mpya, mfumo ulikataa ombi langu kwa sababu bado unanionesha kuwa mimi ni mwanafunzi wa chuo. Nimeendelea kufuatilia ili taarifa zangu zirekebishwe na niweze kuendelea na masomo mwaka huu, lakini hadi sasa sijapata suluhisho, huku muda wa kuanza kwa masomo ukikaribia.
Katika ufuatiliaji wangu, nimekutana na wanafunzi wengine wenye changamoto zinazofanana na yangu. Hali hii inaonesha umuhimu wa kuwepo kwa utaratibu ulio wazi wa kushughulikia wanafunzi waliopata udahili lakini wakashindwa kuanza masomo kwa sababu zisizowahusu.
Ombi langu kwa uongozi wa UDSM na COSS
Naomba viongozi wa chuo pamoja na ofisi zinazohusika na udahili na masuala ya uzamili walifuatilie suala hili kwa haraka, warekebishe changamoto za kiutawala na mifumo zinazotukabili, na kutuwezesha kuendelea na masomo yetu.
Tunatarajia kuanza masomo kuelekea wiki ya kwanza ya Novemba 2026. Hivyo, tunaomba suala hili lishughulikiwe kabla ya muda huo ili sisi tuliopata udahili na kushauriwa kuahirisha masomo tusipoteze nafasi zetu kutokana na changamoto za kiutawala.
Tunaomba ujumbe huu uwafikie viongozi husika ili hatua stahiki zichukuliwe na wanafunzi wenye changamoto hizi wapate ufumbuzi kwa wakati.