Kiutaratibu,mgonjwa hawezi kulaumiwa kwa tatizo alilokuwa nalo.Wote tunaugua,nadhani hakuna atakayefurahi akiambiwa baadhi ya comments zilizotolewa hapo juu
Mkuu wangu usikate tamaa,tatizo lako mimi nahisi sio kubwa sana ila tu halijapata tiba sahihi.Nijuavyo mimi ni kuwa,katika mlolongo wa magonjwa ya zinaa,sidhani kama yanazidi matatu yanayosababisha mkojo kuuma(kwa mwanaume);nayo ni Chlamydia,Gono na Herpes Simplex(HS).Gono na Chlamydia yanatibika kiurahisi kabisa na HS ni self limiting,hata usipotumia dawa inapona yenyewe,.
Nionavyo mimi,wewe hujaenda hospitali ndugu yangu.Inawezekana wewe unaenda dukani,unasema una ugonjwa wa zinaa,wanakupatia Cipro,Metonidazole,Doxycycline,na sindano za Penador,halafu unakuja hapa unasema umetumia kila dawa! Sio kweli mkuu,dawa ni nyingi sana hujazimaliza.Nenda hospitali mkuu utasaidiwa..
Sio kila mtu mkojo unapouma atakuwa na ugonjwa wa zinaa.Kuna magonjwa/matatizo mengine(ambayo sio zinaa) yanayosababisa mkojo kuuma.Mimi nakushauri uachane na dawa za kujinunulia mwenyewe,nenda hospitali ndugu yangu.