Nasumbuliwa na tatizo la Mwili kupata shoti

Nasumbuliwa na tatizo la Mwili kupata shoti

jk1984

Member
Joined
Aug 26, 2024
Posts
11
Reaction score
9
Habari wadau

Nisingependa nieleze sana ila kiufupi napitia wakati mgumu sana nimekuwa nikipata shoti kama ya umeme kwenye mwili wangu kwa muda sasa kwani imekuwa ikitokea mara kwa mara ambapo unaweza isikia mguuni ghafla tena baada ya muda mgongoni na maeneo engine ya mwili jambo hili limenipelekea msongo wa mawazo na kukosa raha kabisa.

Naombeni ushauri maana nimekata Tamaa ya maisha
 
Unahitaji ufatiliaji mzuri ili kujua tatizo la msingi ambayo yaweza kuhusisha:
1: Tatizo la mishipa ya fahamu
2: Madini mwilini
3: Homoni
4: Tatizo la mfumo wa kinga wa mwili

Hivyo:
1: Historia ya ugonjwa ulivyoanza
2: Ukaguzi wa mwili
3: Ufanyiwe vipimo

Mtoa huduma mzuri wa kumuona ni daktari bingwa wa mishipa ya fahamu/neurophysician.
 
Iko hivi kuna watu wana umeme mkubwa kiasi kwamba wanaweza shika umeme wenye volt kubwa sana na hawapigwi shoti kabisa

Kuna wengine anashika tube light na inawaka kabisa,kuna watu wameumbwa tofauti sana au wako special
Dah ama kweli ina maana sisi binadamu wote tuna umeme ndani ya miili yetu ila inatofautiana nguvu?
 
Dah ama kweli ina maana sisi binadamu wote tuna umeme ndani ya miili yetu ila inatofautiana nguvu?
Wote tuna umeme wq kawaida katika miili yetu,ndiyo hiyo inayopeleka signal katika ubongo,mfano ukijichoma na msumar au sindano fasta signal zinapelekwa katika ubongo na unasikia maumivu na kutoa mguu au mkono katoka hatar

Ila hao wengine ni tofauti kabisa,ni wa kipekee
 
Dah ama kweli ina maana sisi binadamu wote tuna umeme ndani ya miili yetu ila inatofautiana nguvu?
Ndio tuna umeme na bila kuwa na umeme mwilini mwako unapata matatizo ya mwili. Ila ukizidi unasababisha matatizo pia ndio maana unashauriwa kukanyaga ardhi peku kwa muda wa dakika 30 kila wiki hasa umri unapoelekea uzeeni hii inasaidia umeme uliozidi upotelee ardhini.
 
Tafuta zile chumvi za Mabonge ogea Kwa siku Saba kisha katoe sadaka ya shukurani baada ya kupona tatizo lako
 
Back
Top Bottom