Nasumubuliwa na tatizo la GERD / Acid reflux

Asante mtaalaamu kwa kuongezea
 
upo sahihi kwenye maelezo, je kwa matumizi ya limau hayatonizidisha tatizo? mana wadau wamenambia niache tumia vitu vyenye acid
Usijaribu kutumia malimao ilihali una acid reflux, kuna watu wamepata acid reflux kwa kunywa malimao wakati mwanzo walikuwa wazima. Shauri ya kusikiliza madaktari uchwara wa mitandaoni
 
Limao italower hydrochloric acid? Chemistry ya wapi hii mkuu? Hivi kama wewe sio mtaalam wa kitu fulani si ukae kimya kuliko kuexpose your ignorance? Kutokujua kitu si dhambi, kama hujui usijioneshe kwamba unajua,hutapungukiwa kitu. Eti na " kuongeza Hydrogen Chloride gas inayokuchoma". Hata hujishtukii
 
Kwahiyo unatarajia weak acid ukichanganya na strong acid concentration ya strong acid itabaki vile vile!!?

Kinachomuunguza ni nini kama sio hydrogen chloride gas inayofanya reflux kwenye umio!!?

Unataka kuniambia ile hydrochloric acid inayozalishwa inaruka kuja kwenye umio!!?
Locally weak acid Ina uwezo wa ku lower concentration ya strong acid


hiyo
 
Kwamba mkuu, weak acid ukichanganya na strong acid,ile strong acid itapungua ukali wake??Tena IN VIVO? Hebu tuandikie equation ya hiyo reaction.
Halafu kinachomuunguza mtu ni acid ndio maana hata dawa wanazopewa ni " anti acid", sio " anti gas". Acid inafikaje kwenye oesophagus? Zile muscles za kuzuia vilivyoko tumboni visirudi juu huwa zimelegea ndio maana hiyo acid inapanda juu na kusababisha hayo matatizo yote.
 
Kwa mwezi wa tatu sasa, nimekuwa nikusumbuliwa na maumivu ya kifua pamoja na kiungulia. Baada kujaribu kulienda deep tatizo nimegundua nasumbuliwa na hilo tatizo.

Naomba msaada wakuu
Pole sana mkuu. Kiungulia na maumivu ya kifua mara nyingi vinaweza kuhusiana na mfumo wa ulaji na mtindo wa maisha. Kwanza, jaribu kuacha kabisa sukari na kupunguza sana vyakula vya wanga kama wali, ugali, mikate, chapati, maandazi na hata maharage kwa kipindi fulani uone mabadiliko. Pia epuka matunda yenye sukari nyingi kama ndizi mbivu na yale yenye asidi nyingi kama machungwa na machenza. Maziwa nayo ni vyema ukayaepuka kwa muda.
Badala yake, kula zaidi protini (samaki, kuku, nyama, mayai, maini), mboga za majani, kabichi, pamoja na parachichi na matango kwa wingi. Haya matunda mawili yawe rafiki zako wa karibu.
Kuhusu mtindo wa maisha, jaribu kula milo miwili tu kwa siku na ufunge angalau masaa 12 kila siku. Mfano, mlo wa kwanza saa 5 asubuhi na wa mwisho saa 10 jioni. Baada ya hapo usile chochote zaidi ya maji. Pia epuka kula mara kwa mara na ukiweza, fanya mfungo wa masaa 24 angalau mara moja kwa wiki (unywe maji tu).
Hata hivyo, kwa kuwa maumivu ya kifua yanaweza pia kuwa dalili ya matatizo mengine muhimu ya kiafya, ni vizuri ukamuona daktari kwa uchunguzi na ushauri zaidi, hasa kama maumivu ni makali, yanarudiarudia, au yanaambatana na dalili nyingine.
 
Na hili ni tatizo la jamii zetu ,juzi binti mmoja aling'atwa na mbwa badala apelekwe hospitali apate matibabu wakaishia kumpakaa mafuta sijui ya nini ,wanajua wenyewe .

Leo dada kapumzika
 
Na hili ni tatizo la jamii zetu ,juzi binti mmoja aling'atwa na mbwa badala apelekwe hospitali apate matibabu wakaishia kumpakaa mafuta sijui ya nini ,wanajua wenyewe .

Leo dada kapumzika
Ila hii nchi, yaani hadi leo hii kuna watu hawajui kama mtu kang'atwa na mbwa kitu cha kwanza ni kumkimbiza hospital haraka? . Mi wakati nakua nimesimuliwa stori watu waliong'atwa na mbwa wakikosa matibabu wanaanza kubweka kama mbwa na kufanya niwe na hofu ingawa sijawahi kushuhudia mtu akifikia hiyo stage ya kubweka. Hao wanafamilia ya huyo binti hizo stori za watu kubweka kama mbwa wao hawajawahi kuzisikia? Kifo cha uzembe kabisa.
 
Mkuu BEZO JR , heshima yako. Mimi ni mgonjwa wa vidonda vya tumbo kwa zaidi ya miaka nane. Baada ya kujaribu tiba mbalimbali na wakati mwingine nilitumia helgo kit lakini kwa siku saba tu sikuendelea nayo tena wala dose nyingine.

Maumivu yalizidi sana bila mafanikio.

Ila baada ya miaka minne numeacha bia, vyakula vinavyonichchea kuumwa kwa tumbo ila linauma-ga pamoja na maumivu ya mgongo.
Na pia wakati nikiwa na hofu na wasiwasi ndo huuma zaidi.

Sijafika stage ya kushindwa kufanya shughuli zangu.


Sasa , niko kwenye dose ya helgo kit nimemaliza dose ya siku 14 na vile vile naendelea na lansoprazole zote hizi ni ushauri niliochukuwa hapa JF na kwa pharmacist.

Baada ya helgo kit niko kwenye dose ya lansoprazole nimefikisha wiki mbili ila bado maumivu yapo. Je kupona kwa vidonda hivi vitachukuwa muda gani mkuu?
 
Dawa pekee ya uhakika ya vidonda vya tumbo ni hot water therapy!!!

Unaianzaje asubuhi yako!

Mchana wako baada ya kula!!?

Wakati unaenda kulala ,mlo wajioni unausindikiza na nini!!??

Ianze asubuhi na maji ya moto kabisa kunywa kama unavyokunywa chai pole pole kama vikombe viwili!! Baadae ndio upate chai na vitafunwa!!mchana ukisha kula unaweza pia ukanywa kidogo walau kikombe kimoja baada ya kula!!

Na usiku pia baada ya kula Fanya hivyo!!iwe sehem ya maisha yako,lakini achana na vinywaji vya baridi kwenye fridge kabisa kama unakunywa kunywa vile vya kawaida kama maji,soda lakini sio baridi kabisa!!


Nilipona kabisa sijawahi kuhisi tena Acid reflux!!
 

Hivi Acid Reflux unaweza kula maharage? Chungwa? Limao? Na usipate shida?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…