Hili suala la Bandari na DP World bado ni bichi na linavuja damu.
Natabiri tu, baada ya muhula wa mama, Prof. Makame Mbarawa anaweza shitakiwa kwa uhujumu uchumi. Prof Mbarawa hana kinga.
Natabiri tu.
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (Tanganyika_Zanzibar) zitapitia wakati mgumu sana kuanzia mwezi Agosti 2023 hadi Julai 2024 katika siasa, kijamii, kiusalama, kiuchumi na kidini
VIASHIRIA
1. Kauli kali zisizo na uvumilivu
2. Matendo maovu baina ya jamii, taasisi na serikali
3. Matumizi na malengo yenye nia ovu kuhusu imani za kidini
4. Itikadi za kimapinduzi dhidi uhafidhina kutamalaki miongoni mwa wana jamii
5. Kubambikiza kesi dhidi ya wananchi wanaoiipa changamoto serikali na taasisi zake tendaji
6. Kuneneana vibaya kati ya makundi kinzani katika itikad za kisiasai na imani za kidini
MATOKEO
1. Visasi
2. Vurugu
3. Kuumizana
4. Kubambikia kesi
5. Mauaji
6. Fitina, majungu na kuchongeana vitaporomosha hadhi na vyeo vya viongozi mbalimbali
7. Ushirikiano kukoma miongoni mwa jamii
8. Kuombeana mabaya
9. Kuviziana na kudhuriana
10. Utawala kuwa hatarini kuondoshwa kwa nguvu ya umma ambayo haijawahi kutokea tangu uhuru
11. Baadhi ya viongozi walioko madarakani, wafanyabiashara na baadhi ya viongozi wa dini kukimbia nchi
SULUHISHO
Kuzungumza kiushirikishi na makundi yote, kukiri makosa, kubadili uongozi, kuthibitisha kila raia ana haki ya kuhoji anachokiona hakina maslahi ya watu na apewe jibu sahihi, kwa wakati na kwa staha ijapokuwa hana cheo chochote (dhamana ya uongozi)