Mambo zenu waTZ wapenda maendeleo kwa mustakabali wa Taifa letu, naanza kwa masikitiko kwani nimefanya investment kubwa bila evaluation, in mwezi uliopita tu nimesajiri jina la biashara BRELA pamoja na changamoto nilizopitia huko lkn namshukuru MUNGU nimefaulu kupata CERTIFICATE OF INCORPORATION. Nikiwa nafanya yote hayo nilishauriwa nitafute mashamba kwa ajiri ya kuandaa raw material kweli nikauza baadhi ya assets zangu nikapata mashamba mawili, zoez lililofuata ni machine za ku process ili nipate bidhaa, nikauliza bei nchini China ilikuwa ni 12M TZ shilling. Sikuwa na shaka sana ikiwa ni pamoja na shipping cost sikuogopa, shida ikaja baada ya kuanza Fanya tathmin uwezo wa machine kula umeme kwa saa pamoja na gharama za vifungashio. Nikauliza uwezo wa machine nikaambiwa ni 15hp saw na 11.2kw maana yake kwa saa natumia unit 11.2 ambazo sawa na sh.4000. Pia bei ya kila kifungashio ni 0.06$ huko China sawa na 138 ya Tz bado sijasafirisha+kodi nikagundua kila kifungashio ili nikipate niwe na kama 220 ukiweka na 18%VAT. nikaja kuchoka baada ya kujua kuwa Daresalam kuna supplier anae import toka China unajumlisha kwa 300 kila packet ya stick, kwa tathmini ya haraka Mimi nikizalisha niuze kila packet moja 800, yani hapa vidonda vya tumbo vinaninyemelea