Natafakari nini cha kumfanya...

Natafakari nini cha kumfanya...

Nasikitika kukwambia hata tuki kushauri utaendelea kua mnyonge wa mapenzi tu.Hauta sikia wala kukoma uta tamani kufanya kitu/jambo ila hauta weza uta baki kutamani tu

Usha ona ayo yote lakini bado humo tuuu
Binadamu tuna kitu kinaitwa hope/matumaini labda atabadilika kwa kujipa moyo lakini mpaka nimeamua kulileta hapa limefika mwisho kwangu moyo wangu ushaingia chuku sana kwa sasa
 
Ngumu kumesa hii

Ndiyo hivyo, watu tunasahau kwamba kuna service tulipata kwenye hayo mahusiano.

Na service hiyo kwa sababu hakuna soko la kupanga bei, tunafikia kutumia ile ya "fair value", ikimaanisha "ulichokubali kulipa kina thamani sawa na ulichopokea".
 
Kwani kuumizwa ni kwenye pesa tu? Hatujui na huyo dada angeumizwa kiasi gani.
Nilichokuja kugundua anajijua ni mzuri sana na anaile character ya wapo wengi wananitaka na ndio ukweli lakn kwa tabia zake ni ngumu kudumu na mtu nimevumilia sababu nilimpenda kweli
 
Habari wanaJf, nitajitaidi kufupisha japo mambo ni mengi sana.
Mwaka jana mwezi wa saba nilifanikiwa kupata mtoto mmoja wa kule milimani akiwa sehemu yake ya kazi akiwa na jiko sehemu flani beach kwa upande wa juu,kiukweli yule binti nirembo sana na yuko very smart and manipulator mzuri sana, mapenzi yalianza kwa mbwebwe mpaka nyumba kwetu na kwao plus mtoto wake na mzazi wake kunijua mambo yalianza kubadilika kidogo kidogo mara ataki Twende wote sehemu mara mawasiliano anachoka sana mpaka awe free by that time nimeshazama mazima, alinichezea mind game moja hatari kuniaminisha she is very innocent na hofu ya Mungu basi nikalibeba ilo lakini chini ya kapeti nasikia story za mtaani kuna jamaa mmoja wa beach flani naye anapiga na wanaonekana nikiuliza nakatiliwa so nikasema sio kesi maisha yaendelee.

This year January akiwa kwao uko milimani siku ya new year nikapewa block moja ya watsap na call nikarudiwa na sababu ya kuwa kuna msiba kwao hakuwa sawa lakini cha ajabu hakujua natumia simu nyingine kuview status zake akiwa anajiachia mahotelini and so ikaenda nikablockiwa tena this time nikaambiwa simu imekufa tukawa tunawasiliana kwa simu yake nyingine up to date, kuna ahadi nilimpa kwa kweli imekuwa kama fimbo na imeonyesha yuko interest ya iyo ahadi kuliko ata mimi muhusika nilichofanya nikawa natoa kidogo kidogo, inafika mda iyo simu nyingine nayo inazimwa pia kwaiyo imekuwa vurugu kabsa ndani ya moyo.Mda wote huu mimi ndio nilikuwa na sponsor kila kitu mtaji, pocket money, hela ya kula nyumbani, kodi ata ada ya mtoto na vitu vinge vidogo vidogo.

Maswali ninayo mengi sana kichwani kosa langu liko wapi na mbona hakuwa muwazi toka mwanzo nipite nisepe zangu i dedicated my self kwenye hayo mahusiano kujua nimepata mke bora kabsa nimejikuta nimeingia kwenye madeni yasio na misingi yote kujaribu kumridhisha.Sio kwamba nimekosa mwanamke wakunipenda au sina muonekano ila nimeamua kutulia naye tuanze maisha kwa kweli haya mambo yasikieni kwa mwenzako nimepoteza kilo za kutosha nimejikuta nimetumia zaidi ya 10M ndani ya miezi 6.Nimegombana na washkaji na ndugu sababu yake nikiamini hawamjui vzuri lakn makucha yake nimekuja kuona mwisho.

Wanajf naombeni mnipe muongozo kwenu nimeingiwa na chuki sana sijawai mfanyia mtu baya lakini this time am ready ata kuroga,kama mtu akuwa na huruma na utu juu yako unakuwa kuwaje na huruma kwake,nimejikuta natafakari mengi sana labda ndio tabia yake kucheza na hisia za watu nakuamia kwa mwingine kwa sababu kwa sasa nimemwambia sina kitu ameamua kukaa kimya na simu inazimwa mda mwingine, kuna mtu kaingia mkenge tena nadhani sasa huyu kawa janga la taifa inaweza mkuta mdogo wako au ndugu yako tusitumie jazba wala matusi,i admit she caught me off guard kabsa with the ability she as ni tatizo.
Single mother huwajuii wewe mbona bado narudia NA BADO
 
Mimi nikikwazwa hua naachia ngazi kimya kimya halafu yeye ndio aanze kuhangaika na maswali ya kinafiki “ eti mbona sikuelewi etc”

Napotezea mazima. Hii njia nimeibuni baada ya kupitia mashida kama yako. Cha msingi ni kuwa kuhonga ni kwa kiwango kidogo sana kwa ajili ya kusogeza maisha tu, ili hata mambo yakivunjika maumivu yasiwe makubwa
Hongera kwa ubunifu mkuu
 
Back
Top Bottom