Ushauri wangu unalenga Kwa vyote viwili, yaani Kwa aliye na mtaji na Akina Pangu pakavu. Lakini Kwa Akina Pangu pakavu Tia mchuzi' ndipo mahali pakutobolea.
Kwanza hakuna mtu wala taasisi ya fedha inayompa Mkopo mtu asiyekuwa na cents za kuanzia yeye mwenyewe. Hivyo basi Pangu Pakavu akishalijua Hilo Hana HAJA ya kuwa na shida ya mafanikio ya haraka sababu Hana huo uwezo. Anatakiwa apange mipango ya muda Mrefu 'Long term Plans' kutegemea na ulichonacho Binafsi pasipo kuomba Mkopo kokote kule, jasho lako Tu Kwa kuanzia litakupa mafanikio iwapo utakuwa na mipango ya muda Mrefu.
NI kwanini iwe ' Long term Plans' sababu huna kitu na hata iweje uwezi fanikiwa Kwa muda mfupi! Matokeo yake utaishia kuhesabu siku Tu, wiki, miezi Hadi miaka utakuwa pale pale Tu. Kama huna mtaji na wala huna assets basi 'Komaa' Kwa nguvu na akili zako Kwanza ili update kianzio. Tatizo linalosumbua NI kwamba unataka ufanikiwe haraka haraka wakati mtaji haupo. Karibu Kwa ushauri