Natafuta ajira, nimeambatanisha na CV yangu

Umeandika vizuri sana Boss ngoja nikueleze jambo kidogo, niliwahi kupewa contract katika moja ya vituo vya redio mkoani na nilivofika tu ndani ya wiki 2 nikaleta maendeleo chanya kiasi cha kupewa U programm manager. Ila baada ya miezi kama 6 redio ile iliuzwa kwa moja ya kiongozi wa dini hapa nchini na akaweka utaratiu wake mpya na kutangaza hadharani kuwa yeye haangalii degree ya mtu anachotaka vipindi vyake vya dini tu viende mbele na yupo tayari aweke hata mtu wa darasa la saba afanye kazi ya kupandisha na kushusha feda (Kuwasha microphone na radio kuwa live) muda tu yeye anapotoa mahubiri. So from there option ilikuwa moja tu uondoke mwenyewe au ubaki na hulipwi. Social media zote zinakuwa managed kutoka makao makuu Dar, posters zote na videos as well


Kazi zingine nimezifanya as Freelancer na ndo hizo zananiweka mjini ila shida hazina consistency na nazifanya na wanafunzi sanasana, so kupitia recommendations zao hela za hapa na pale zinapatikana. Mfano humu Jamii Forums kuna watu nilishafanya nao na wakanipa recommmendations kwa wanafunzi wenzao na nikafanya kazi nao, shida ni kuwa hazina consistency, so waweza kuta kwa miezi miwili umefanya kazi 2 au moja (Consistency is the key)


Kwa upande wa watu binafsi na Taasisi nilizofanya nazo kazi kuanzia hizo District na Municipal waliniambia una potential kubwa ila shida nafasi unayotakiwa ukae wewe ina mtu ambaye anafanya vetting na yeye anawatu wake hivyo ni ngumu (Nilitamkiwa haya maneno live, face to face), upande mwingine wa Ajira portal nako nimeshafanya interview 2 nako bila bila.

Naamini nimejibu hoja yako kama kuna swali jingine ntakujibu
 
University of Tanzania kipo wapi hiki Chuo? Hizo kazi ambazo umefanya si ndo ungeweka hapa samples. Mabango na videos. Tuone kazi zako?
 
Uko vizuri sana Mungu akutangulie πŸ‘πŸ»πŸ‘πŸ»πŸ‘πŸ»
 
Umegraduate UNIVERSITY OF TANZANIA IPO WAPI?

usitaje taasisi ulizofanya kazi. Onesha kazi uliyofanya
Nakupa mfano nina research za watu zaidi ya 100 nitaziweka hapa?? nina proposal za taasisi zikiomba mikopo nitaziweka hapa? nina video ziko youtube pia siwezi kuziweka hapa, ndio maana wanaokuja PM nawaonesha hizo kazi sababu nyingine ni confidential Boss, ngoja niombe ruhusa kwa baadhi ya wateja wangu then niweke hapa manake nyingine sio za matangazo
 
Unazunguka sana. Yaani kwa maelezo na uzoefu wako hukupaswa ujieleze sana. Ungetupia video clip moja au mbili, ungetupia mabango au flyers ambazo umetengeneza maana hizo si za kuficha. Weka kazi ulizofanya ndugu hizo si siri.
 
Ambazo si za matangazo kama biz cards hizo usiweke. But kama ni mabango ficha jina au some details. Tuone art yako na graphics. Research proposal usiweke. Kuna kazi ambazo ukiweka hapa hazina athari kwa wahusika. Tuone kazi zako.
 
Ambazo si za matangazo kama biz cards hizo usiweke. But kama ni mabango ficha jina au some details. Tuone art yako na graphics. Research proposal usiweke. Kuna kazi ambazo ukiweka hapa hazina athari kwa wahusika. Tuone kazi zako.
Ngoja naziattach pale juu ya uzi soon
 
Ambazo si za matangazo kama biz cards hizo usiweke. But kama ni mabango ficha jina au some details. Tuone art yako na graphics. Research proposal usiweke. Kuna kazi ambazo ukiweka hapa hazina athari kwa wahusika. Tuone kazi zako.
Nenda juu ya uzi pale kuna ambazo nime attach 2 ni recently, 2 ni za 2022
 
Nenda juu ya uzi pale kuna ambazo nime attach 2 ni recently, 2 ni za 2022
Safi sana. Ndo nlitaka hivyo. Weka na video nataka watu waone kazi zako. Hiyo ndo CV kubwa zaidi kuliko ile uliyoandika. Actions speak louder than words.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…