Natafuta business partner wa information technology company

Natafuta business partner wa information technology company

Joined
Feb 7, 2015
Posts
30
Reaction score
12
Habari wana JF,
Mimi ni Mjasiriamali mwenye umri wa 20' yrs.
Nimesoma Bachelor of Science in Computer Science Software Engineering, nimejiajiri kwenye industry ya IT.

Nimefungua ofisi Sinza Makaburini mtaa wa sokoni. Ofisi imesajiliwa Brela na TRA, pia ofisi ina furniture (Meza za ofisi Mbili, Viti vya ofisi viwili, Viti vya kukaa wateja vitatu, Computer Desktop 1, Office jet Printer 1)

Ofisi ina mazingira mazuri sana na ipo sehemu nzuri na tayari inafanya kazi kwa takribani miezi mi4 na ina wateja.

HIVYO BASI:
Nahitaji mtu mmoja (1) mwenye mitazamo chanya ya kibiashara kushirikiana nae kwenye ofisi hii, awe na vigezo vifuatavyo;
  1. Awe na Taaluma ya Computer Science, Computer Engineering, IT au Software Engineering
  2. Awe na uwezo wa kufanya vitu na siyo mzuri wa kueleza NOTES zinasema nini hasa katika sehemu hizi; Software Development, Networking, Pc Maintenance, na Entrepreneurship na Good Customer Care
  3. Awe na kazi kama mifano ambazo alishawahi kufanya
  4. Asiwe ameajiriwa au mwenye mawazo ya kuajiriwa hivyo kukwamisha malengo tutakayojiwekea
  5. Awe ana uwezo wa kufanya kazi katika mazingira magumu, hasa wakati wa kutafuta wateja na kipindi cha wateja wachache/hakuna
  6. Awe na Ujasiri wa kufanya biashara na kuthubutu hata palipo na hali ngumu

JINSI YA USHIRIKA
  1. Mtu huyu atakuwa sehemu ya Partnership kihalali na tutashirikiana katika kila Jambo la ofisi.
  2. Mapato yatakayopatikana yatakuwa ni ya ofisi, na faida tutagawana sawa kipindi tutakapoona inafaa kugawana kulingana na mipango ya ofisi
  3. Tutashirikiana kuandaa mikakati ya jinsi ya kupata wateja na kukuza ofisi zaidi

NINI KINAHITAJIKA TOKA KWAKE:
  1. Mshirika huyu atatakiwa kuwa na Computer either Desktop or Laptop yenye uwezo mkubwa wa kufanya kazi na kuhifadhi data
  2. Awe na Mchango kama sehemu ya mchango wake wa kodi. Kiasi cha Tsh. 360,000/- (Kodi ya Miezi 6, March - August)
  3. Aje na vyeti katika kozi tajwa hapo juu kuthibitisha elimu yake (Itasaidia kuandaa Company Profile na sifa za watendaji wakuu)
  4. Utayari wa kuanza kazi kwa moyo mmoja na ujasiri wa hali ya juu.

MAWASILIANO:
Kwa mawasiliano zaidi, Nipigie kwenye
0713 741 758





 
Hongera sana kwa kuweza kujiajiri. Nina maswali mawili,
1. Umesoma wapi degree yako?
2. Mbona unafunga milango kwa watu wengine?

Kwanini nimeuliza swali la 2. Kwa sababu nchi za dunia ya tatu ndio zenye uchumi unaokua kwa kasi. With your background in software you can make miracles if you come up with solutions in different areas.
 
Back
Top Bottom