Natafuta Business Partner

Natafuta Business Partner

Nataka hisa asilimia 51, je upo tayar..?
 
Nina uzoefu wa miaka karibu 8 na nina kampuni iliyosajiliwa rasmi. Kampuni inashughulika na mambo ya Media/Broadcasting/Video Production. Pia nina vifaa ila nina mambo mawili matatu ya kuongeza ili kufanya kazi kwa ufanisi. Kwa miaka yote pesa niliyokuwa napata nilikuwa naitumia kununua vifaa zaidi ila kwa kweli nahitaji some support ili kuvuka hili daraja lililo mbele yangu. Tukivuka hapa tulipo, naamini sky is the limit.

Ninahitaji mtu atakayenisaidia kuniongezea mtaji na makubaliano ni kugawana faida kwa mwaka mmoja (au muda wowote tutakaokubaliana) katika mgawanyo tutakaokubaliana toka mwanzo. Baada ya muda tutakaokubaliana, tunaweza kuamua ku-extend mkataba, kuubadilisha, kuuvunja au hata kuuweka permament. Haya yote yatategemea na makubaliano kati yetu.

Kama nilivyosema, kuna mambo machache yananikwamisha lakini kama nikipata mtu serious na mwaminifu, yanatatulika. Niko tayari kupokea ushauri wowote wenye nia ya kujenga.

Nipo tayari kuonyesha kazi nilizofanya, mipango ya muda mfupi na mrefu, assets za kampuni, n.k. Kampuni haina madeni.

Ninachotafuta:
  • Kwa makadirio, nahitaji ongezeko la mtaji la kama milioni 10 (60% itakuwa ni kuongeza vifaa na inayobaki ni working capital). Tukikaa chini nitatoa mchanganuo rasmi.
  • Mtu ambaye yuko open-minded na awe na contacts tutakazoweza kuzitumia kupata wateja. Ningependa vilevile aje kuwa active kwenye shughuli za kampuni hasa katika mambo ya marketing. Mambo ya Technical naweza kuyashughulikia mimi.
Uko wapi mkuu? Na unapatikanajee
 
We
Kama umekubaliana na maelezo yangu yote, ikiwepo kwamba mkataba wa kwanza ni wa muda maalumu na vilevile ushiriki wako katika biashara, tunaweza kuongea.

Nadhani ulikuwa unamaanisha mgawanyo wa faida wa 51%. Itabidi niombe ushauri wa kisheria kujua hii kitu inaweza kuwekwaje.

Tuwasiliane kwenye PM.
Unataka kupewa mtaji lakini hutaki kuuza hisa endelea kusubiriii. Je ndani ya mwaka utarudisha huo wa 10 m iwapo hutataka kuongeza mkataba? Ina maana mimi nitapoteza pesa zangu nilizoweka kwenye kampuni yako. Maan unaongelea kugawana faida ila huongelei mtaji wa mwanzo unakuwa mali ya nani??
 
Mi naona anaongelea faida tu!!!kuhusu pesa ya mwanzo inajulikana waz lazima irudi.
 
Back
Top Bottom