Natafuta Contacts za Dj Mark, yule anaetafsiri Movies kwa Kiswahili

Hua anafurahishaa yupo na yule anaitwa dj mafi nadhana yule kiboko anachekeshaa balaaa alitafsiri arrow on the bowstring nadhan ni kibokoooo

Kumbe dj mafi na dj mark ni watu wawili tufauti???nilikuwa sijui..mbona wanafanana sana sauti??
 
Umenikosha sana mleta mada yaani pamoja na maisha yangu ya sasa lakini sisahau asili yangu ya kuangalia movies kwenye mabanda tena za dj mark huwa nafarijika sana ila nikikua nitaacha.

mi enzi zangu za lufufu
ila hawa bwana sound nyingii kwenye kihindi
siku hizi kuna juma khan,tariq aziz na dj mark hao ndo maarufu maarufu
 
DJ mark ndo king wetu wa banda umiza yaaani ata nikae na niende WAP lazma niangalie muvi alioitafsiri dj mark wa acheche production mtoni mtongani.
 
Huyu Mafi na dj mack hua hawadnganyi sema kuna kunogesha fulani hivi sasa wapo wale yaan full kudanganyaa subtitle haiendan na anachotafsirii

DJ mark hatari, tupuu Kama sikoseii jamaa alianzia Arusha alikua na mabanda mawili ya kuonyeshea movies na hope ilikua around 2002-8, yaani akitafsirii yeyee jamaa anajazaa mpka watu wanakosa pa kukaa wanasimama mlangonii! Na kila SAA mbili usiku ilikua ni movie za Kihindi mpka saa 6 usiku basi UNTY yangu alikua anapendaa Sana I remember one day akanichuka na kunipelekaa kuangaliaa movie ya kihindii inaitwa ""ANDHA KANOON"" under translation ya Dj mark duuuuuuuuh!!!! Nililiaaa mbayaa mno nikaanza jifuta machozii kujaa kutizama pembenii raiaa wote pia wanaliaaa yaani nilichekaa Sana,

Ila kiukwelii ilikua ni poa Sana enzi zilee kumsikizaa dj mark, ndio baadae akasepaa na kuja daslamm basii bwanaa na movies za kihindii zikaishia hapooo 😁😁😁
 
Huwa unajisikiaje Dj mark akitafsiri movie ya vita ya kimarekani au ile waarabu ya kivita hahahahahahaha utafurahi hadi basi ame tafsiri expendable 3 utasikia haya sasa kama kipelee kimepata mkunaji anakujaaaaaaaaaaa ( ile sehemu jamaa anaendesha pikipiki hatareee angekuwa bodaboda yule sijui ingekuwaje)
 
Mimi toka nifahamu kikristo, nikiona movie imetafsiriwa uwa siwezi angalia hata iwe ya kikorea naona bora nidownload subtitles.
Unless iwe imetafsiriwa kama zile tamthilia za kichina zinazoinyeshwa tbc za akina maudodo
 
Mimi toka nifahamu kikristo, nikiona movie imetafsiriwa uwa siwezi angalia hata iwe ya kikorea naona bora nidownload subtitles.
Unless iwe imetafsiriwa kama zile tamthilia za kichina zinazoinyeshwa tbc za akina maudodo

Nimepata tabu kukuelewa kikristo unamanisha nini nikajua umeokoka ila sasa nimekuelewa si ndo ule ugonjwa wa yule mchezaji mkubwa wa machester united anaitwa Valencia ambao unamsumbua lakini wewe hapana hahahahahah
 
Mpe wasifu wake unaomstahili...unahitaji contacts za HARAMIA au FISADI Dj Mark.

Anachofanya ni kudhulumu kazi za wenyewe, yaani wengine waumize vichwa mpaka kazi itoke hivyo unavyoiona, then wewe uje tu na kuigeuza dili lako....hana tofauti na anavyofanya yule NYOKA MWENYE MAKENGEZA.
 

Ulitaka aue albino au awe jambazi anajitafutia bana kutafsiri napo ni kazi mnoo
 
Aaaaarg hizo movie's zilizotafsiriwa sizipendi kabisa.Mimi hasa kwenye za kikorea nataka nikisikie kile kikorea.
Ngoja waje wenzio labda watakusaidia.

Mbna hzo za kikorea ndo anapatiaga sana kuztafsir eb angalia jumong,nine,joseon the gun man&dong yi uone
 
Nimepata tabu kukuelewa kikristo unamanisha nini nikajua umeokoka ila sasa nimekuelewa si ndo ule ugonjwa wa yule mchezaji mkubwa wa machester united anaitwa Valencia ambao unamsumbua lakini wewe hapana hahahahahah

Hahaha mkuu nimekuta nacheka kweli baaa ya kusoma comment yako na kuitafakari
 
kuna pimbi mmoja wa arusha naye anatafsiri dah!anazidi kuwafanya waarusha waonekane mapimbi maana ana lafudhi ya kiboya halafu anajaribu kutaka kupita wanapopita wakali kina lufufu
 
Ulitaka aue albino au awe jambazi anajitafutia bana kutafsiri napo ni kazi mnoo

Huwa kuna utaratibu maalumu unafuatwa iwapo unataka "kuhariri upya" kazi ya mtu mwingine....tusihalalishe uhalifu kwa kuwa tu anayeibiwa hayupo hapo karibu na wewe....

Tukimpongeza kwa anachofanya basi tuwapongeze pia na wakwepa kodi, mafisadi na matapeli wote.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…