Natafuta darasa special la kiingereza

jerry monny

Member
Joined
Dec 6, 2010
Posts
94
Reaction score
0
nipo arusha,kunarafiki yangu anatafuta darasa maalum kwa ajili yakujifunza lugha ya kingereza.vyuo vipo vingi sana kwa sasahivi yupo pale jengo la molell alakini hakuridhika na mafunzo anayopata.tafadhali kwa anaefahamu wapi lilipo chuo,shule,au mwalimu mzuri wa kumsaidia.bei watapatana hili halina tatizo.naombeni msaada wenu.asante.
 
Aende British Council ila sidhani kama Arusha wapo. Dar ipo karibu sana na Steers & CRDB Holland Branch.
 
Naomba kujua hapo Bitrish Bei gani kwa course
 
nashukuru.kuja dar hatoweza kwani mfadhili wake budget yake hatoweza kukidhi maisha ya bongo.isitoshe jamaa anafamilia huku,inabidi kila mwisho wa wiki akaisabahi familia ya yake,thanks for ur concern.
 

Ndugu yangu lugha ni mazoezi, anao uwezo wa kujifunza kimombo bila hata mwalimu, kwani mwalimu wake wa kiswahili na kinyumbani alikuwa nani, anamkumbuka, badala ya kukaa na kusubiri mwalimu na shule nzuri aanza sasa kwa kusoma machapisho ya kiingereza hata kama haelewi, kusikiliza redio za kiingereza kuangalia TV kwa kiingereza ataanza kujua maana ya neno mojamoja na jinsi ya kutamka, ni lazima ajenge mapenzi ya dhati na lugha hiyo, asione aibu kuizungumza hata kama ni broken, pia asidanganyike na yale matangazo ya ONGEA KIINGEREZA KATIKA WIKI MBILI hakuna kitu kama hicho. Mwambie maana akikijua kitamsaidia kwa mengi. ingawa kujua kiingereza sio kuelimika
 
Jamaa mwenyewe hata kiswahili chenyewe mzozo,duh!poa alakini ngoja aendelee na hapo alipo then ata seach huko mbele.
 
Lukansola kweli umenena,siri ya lugha yeyote kwanza ni muhusika kuamini kuwa anaweza,shule nikwenda tu kupata msingi lkn mafanikio yatakuja kwa bidii binafsi hasa kusikiliza redio ktk lugha uitakayo tv nk
 
Hiyo ni gea na wala si rafikie jua mficha maradhi ni vigumu kupona sema ni wewe au tuambie matembele kwa kiinglish ni nn? ili tuamini
 
Kama ungelikuwa wewe ningekupa njia rahisi ya kujifunza lugha kwa njia rahisi kabisa bila ya kupoteza pesa zako bure.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…