Natafuta Dawa ya Panya

Natafuta Dawa ya Panya

Nikiangalia Comment za watu wengi Humu ndani naishia kujiskia vibaya kama vile mimi ni muuliza swali,kiukweli sijajua tatizo la JF hii hadi leo,maana kipindi cha nyuma kidogo ukiuliza swali kama hili ilikua lazma upate solution nzuri..ila nowdays ni utani,kejeli na dhihaka mno kuuliza swali JF,kama mtu hajauliza swali kwa Utani au dhihaka kwann umjibu hivyo? Si ustaarabu hata kidogo, tujifunze kunyamaza pale ambapo tunaweza kuwakwaza watu wengine..hasa wenye Matatizo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tatizo Watoto wamejaa sana humu ndani kwa sasa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu jambo la kwanza ni usafi wa nyumba yako na kupanga vitu vizuri,usijaze makorokoro ndani maana humo ndio huwa wanapenda kujificha na kama unauwezo unaweza kufuga paka maana naye anahitaji matunzo.

-Ndumilakuwili-
 
Tumia vidonge vya Indocid kwa kuweka ktk nyanya

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu nahisi hujamuelewa mtoa mada

Hataki kutumia sumu, anatafuta dawa ya kuwafukuza tu

Indocid ukiweka wanakula ukichochanganya na hiyo dawa halaf ikisha wanafia mafichoni humo humo ndani mkuu

Me nahisi dawa ya hawa viumbe ni kujipangilia vyema ndani mwako, kupanga vitu vyako kwa hali ya usafi na mtiririko mzuri

Madame S
 
dawa ya panya ni kufuga paka ila kama wewe ni msela kigeto geto paka utamtesa tu bora ununue sumu.

Sent from my Siemens kidole juu using JamiiForum mobile app.
hawa paka wa mjini chenga sana,wangu anajifanya hali panya,hata akimuua anamchezea afu anasepa,ye anakunywa maziwa tu na nyama ya kupikwa
 
Back
Top Bottom