Natafuta Guest House inayoanzia 10,000-20,000 Dodoma Mjini

Wengi mmejikita kwenye kigezo cha bei na jina LA lodge mkasahau sharti LA msingi LA mtoa mada 'Pasiwe na wanawake wanaojiuza' nikabaini kumbe kigezo cha msingi ni wanawake wanaojiuza. Mtu asiyekuwa na shida nao huwa haangaiki nao, mtoa hoja anawatafuta kwa kunena kinyume chake hivyo muelekezeni walipo
 
Naona watu wanakupoteza hapa. Kuna fact zifuatazo unatakiwa uzijue kuhusu Dodoma;
1. Stand ilipo hakuna guest hata moja iko nje ya mji.
2. Kutoka stand ilipo kwenda mjini katikati ni umbali wa dak 30 hadi 45 kwa daladala za kawaida.

Hivyo kwa maana hiyo mtu akikutajia guest ambayo iko karibu na stand anakudanganya.

Unachotakiwa kufanya. Ukifika stand kuu Dodoma waambie wakushushe mjini (Makole au CBE, ukishashushwa hapo kuna ofisi nyingi za mabasi ya kwenda Mwanza ambayo asubuhi hata usipoenda stnd kuu unaweza pandia hapo, watakupa maelekezo.

Pia hapo hapo maeneo hayo luna guest nyingi sana ambazo zitakuwa za karibu na bei yeyote utakayotaka.

Angalizo: maeneo haya pia ndio Bunge lipo, so kunauwezekano pamejaa sana lakini ukifika mapema ni rahisi kupata sehemu nzuri na ya na ya bei unayotaka wewe.
 
Mtu anayeulizia bei za vyumba vya kulala namfananisha na mtu anayeingia hotel na kuanza kuuliza @ misosi na bei zake..hD soda atauliza..kwahyo ukiniletea ugali mboga mbog na soda inakuwa sh ngap🤔🤔!heee hapa soda mnauza 700???🤔🤔!
 
Asante sana mkuu kwa ufafanuzi murua
 
Ni vema kuuliza kuliko kuingia kichwakichwa tu.
 
Maili2 ni kabla ya stand 88 au baada kama umetokea Dar?
Maili mbili uko uelekeo mwingine kabisa... Maili mbili ipo kama unaenda Arusha kupitia Kondoa...

Au kama unaenda Chuo cha Mipango.
 
Unaenda Katavi bilashaka ni Mpanda then ukapumzike Dodoma! Kwann usipimzike Tabora kwasabb unaweza kujikuta unalala tena Tabora kwasabb kutoka dom mpaka Tabora utafika mchana sana hakutakuwa na Gari la kukufanya uendelee na safari! Ushauri wangu kapumzike Tabora
 
Asante kwa ushauri mzuri lakini lengo kuu la kupumzika Dodoma ni la kiutalii zaidi,ili nipate cha kusimulia siku za usoni.
 
I reserve this comment,itanifaa siku za baadae ubarikiwe sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…