Natafuta Huduma ya Akiba ya Fixed Term Inayoruhusu Kuweka Mara kwa Mara Bila Kutoa Mpaka Muda Uishe

Natafuta Huduma ya Akiba ya Fixed Term Inayoruhusu Kuweka Mara kwa Mara Bila Kutoa Mpaka Muda Uishe

hyle master

JF-Expert Member
Joined
Jan 27, 2013
Posts
209
Reaction score
23
Wakuu habari,

Naomba msaada wa maarifa kutoka kwa yeyote anayeifahamu huduma ya benki au mobile money inayoruhusu kuweka akiba ya muda maalum (fixed-term saving) kwa mfumo ufuatao:

Nijiwekee muda mfano mwezi 1 hadi mwaka 1

Niwe na uwezo wa kufanya deposit mara kwa mara wakati wa kipindi hicho

Nisiweze kutoa pesa hadi kipindi hicho kimalizike (strict lock-in)


Nimejaribu baadhi ya huduma kama:
📌 Tigo Pesa Kibubu
📌 Vodacom Mgodi
📌 Selcom Kibubu

Tatizo ni kuwa huduma nyingi kati ya hizi:

Zinaruhusu kuweka pesa mara moja tu kwa saving ya muda maalum

Au hazina lock period – unaweza kutoa muda wowote


Kama kuna yeyote anayefahamu huduma bora ya aina hii (iwe ya benki au mobile wallet), tafadhali naomba ushauri.

Asanteni sana.
 
Umenikumbusha kudumbukiza Chochote uko UTT, Jamani ukiwa unajitafuta kuserve ni ngumu sana
 
Back
Top Bottom