Wakuu habari,
Naomba msaada wa maarifa kutoka kwa yeyote anayeifahamu huduma ya benki au mobile money inayoruhusu kuweka akiba ya muda maalum (fixed-term saving) kwa mfumo ufuatao:
Nijiwekee muda mfano mwezi 1 hadi mwaka 1
Niwe na uwezo wa kufanya deposit mara kwa mara wakati wa kipindi hicho
Nisiweze kutoa pesa hadi kipindi hicho kimalizike (strict lock-in)
Nimejaribu baadhi ya huduma kama:
π Tigo Pesa Kibubu
π Vodacom Mgodi
π Selcom Kibubu
Tatizo ni kuwa huduma nyingi kati ya hizi:
Zinaruhusu kuweka pesa mara moja tu kwa saving ya muda maalum
Au hazina lock period β unaweza kutoa muda wowote
Kama kuna yeyote anayefahamu huduma bora ya aina hii (iwe ya benki au mobile wallet), tafadhali naomba ushauri.
Asanteni sana.